Presha ya Kushuka: Dalili, Sababu, Huduma ya Kwanza na Namna ya Kujidhibiti

Presha ya Kushuka ni Nini?

Presha ya kushuka (hypotension) hutokea pale shinikizo la damu linapokuwa chini ya kiwango cha kawaida – chini ya 90/60 mmHg.

Hii husababisha damu kushindwa kufika sehemu muhimu kama ubongo, moyo, figo, na kusababisha hatari kubwa kiafya.

Cover

Pakuwa Pdf Free! Vyakula kwa Presha ya Kushuka

Kwa Nini Presha ya Kushuka Ni Hatari?

Watu wengi hudhani presha ni ya kupanda tu – kumbe presha ya kushuka pia ni hatari, na mara nyingi haina dalili za wazi. Ndio maana huitwa muuaji kimya kimya.

Dalili zake zinaweza kuonekana kama kisukari kushuka, uchovu au kizunguzungu – hivyo ni rahisi kuchanganya tatizo.

πŸ‘‰ Soma pia: Dalili za presha ya kupanda na madhara yake

Dalili za Presha ya Kushuka

Unaweza kuwa na dalili zifuatazo presha yako ikishuka

DaliliInaaza kwaHatari Gani?
KizunguzunguMara moja ghaflaKuanguka na kupoteza fahamu
Kichwa chepesiKusimama ghaflaKukosa hewa ya kutosha ubongoni
Kushindwa kuona vizuriBaada ya kusimamaUsalama barabarani/ajali
Moyo kwenda mbioBila sababuMsongo wa mawazo
UchovuSiku nzimaKupungua uzalishaji kazini

Sababu Kuu za Presha Kushuka

Sababu za presha kushuka zinaweza kuwa zifuatazo:

  1. Upungufu wa maji mwilini
  2. Kusimama kwa ghafla (orthostatic hypotension)
  3. Matumizi ya dawa za presha au kisukari
  4. Hali ya hewa ya joto kali
  5. Magonjwa ya moyo
  6. Magonjwa ya figo
  7. Sukari kushuka (hypoglycemia)
  8. Msongo wa mawazo
  9. Lishe duni / kupungua uzito ghafla

Jinsi ya Kutofautisha na Sukari Kushuka

Watu wengi hupima presha tu β€” bila kupima sukari.

Dalili za presha kushuka ZINAFANANA na sukari kushuka – hivyo ni hatari kuchukua hatua bila kujua chanzo.

πŸ“Œ Suluhisho: pima presha na sukari mara 2-3 kwa siku kwa wiki 1.

πŸ‘‰ Soma zaidi: Namna ya kupima presha na sukari nyumbani


Huduma ya Kwanza – Presha Ikishuka Ghafla

Ukipatwa na presha ya kushuka ghafla, huduma ya kwanza ya presha ya kushuka ni muhimu sana ili kuzuia madhara kwenye ubongo na moyo.

Hapa chini ni hatua za haraka unazopaswa kuchukua kama first aid ya presha ya kushuka

  1. Omba msaada kwa kuita watu wengine
  2. Lala chali na nyanyua miguu juu
  3. Pumua taratibu
  4. Kunywa maji YA KUTOSHA
  5. Tumia maji + chumvi kidogo (ORS)
  6. Usisimame haraka
  7. Epuka kusimama muda mrefu
  8. Pima presha & sukari mara moja

Vyakula vya mtu mwenye presha ya kushuka

Hapa nimekuandikia vyakula vya mtu mwenye presha ya kushuka vinavyoweza kukusaidia kupandisha presha yako kwa kiasi kizuri. Hatahivyo, vyakula hivi havitibu tatizo – vinasaidia kwa MUDA tu.

Aina ya ChakulaKwa Nini Kinafanya Kazi
ORS / maji yenye chumviHuongeza blood volume
Karanga & njuguHealthy fats zinasaidia moyo
Supu ya mifupa / MakongoroHurejesha madini chumvi (electrolytes)
Ndizi / viaziPotassium na sodium balance
Mayai & samakiProtein + omega 3

πŸ‘‰ Unahitaji lishe maalum ya kudhibiti presha?
Pata Kitabu cha Lishe ya Presha hapa

Nini Cha Kufanya Ili Kudhibiti Presha ya Kushuka

HATUA 4 ZA KUANZA LEO

  1. Fahamu baseline ya presha yako
  2. Rekodi vipimo kwa wiki moja
  3. Chunguza chanzo kwa uchunguzi wa kitabibu
  4. Jifunze mbinu za kudhibiti presha kisayansi

PreshaPlan – Mfumo Unaokusaidia Kujidhibiti

Katika PreshaPlan, utapata:
βœ” mafunzo ya kisayansi
βœ” njia za kudhibiti presha bila hofu
βœ” maelezo ya kutofautisha presha & sukari
βœ” ushauri binafsi kutoka kwa Dr. Adinan

πŸ‘‰ Bonyeza hapa kujiunga na PreshaPlan

Scroll to Top