PreshaPlan

Zaidi ya Asilimia 95% ya Wagonjwa Wetu Wanadhibiti Presha Ndani ya Mwezi 1

Tunakurudishia Amani kwa Kukuepusha na Madhara ya Presha kwa Kukupatia

📚 Elimu Sahihi
🥗 Maamuzi sahihi kwa wakati
📊 Tathmini ya Ufanisi

Sababu 3 Uko kwenye Hatari Ya Kupata Madahara ya Presha

Ni wagonjwa 23 tu kati ya wagonjwa 100 wanaopata matibabu ya Presha wamefanikiwa kudhibiti presha zao. Hii inamaanisha watu 77 waliobaki, licha ya kuwa wanatibiwa wako kwenye hatari ya kupata madhara makubwa kama vile figo kufeli, moyo kutanuka, au kiharusi (stroke).

Hizi ndizo Changamoto kuu 3 zinazokuweka kwenye Hatari:

1

Huujui Ugonjwa wa Presha

Athari kubwa ni Kuyumbishwa. Kila mtu anasema lake na wewe unafuata. Ingawa lengo lako ni kuepuka madhara. Miluzi mingi hupoteza mbwa. Lakini kwakuwa umefika hapa sasa uko makini na utafanikiwa.

Ushahidi: Umeugua muda mrefu lakini mpaka sasa unaulizia kama unaweza kuacha dawa presha ikikaa sawa, au hujui nini cha kufanya nyumbani presha yako ikipanda sana. Au kusema “vyakula vya mgonjwa wa presha ni ghali”.

Unavyotakiwa uwe kuanzia leo: Ufahamu timamu wa uhakika unaokuwezesha kufanya mambo na kuona matokeo chanya:

2

Hufahamu Kiwango Chako cha Presha – Muda mwingi

Athari kubwa: Kupata madhara taratibu na kuyatambua wakati hali imekuwa mbaya.

Ushahidi: Wagonjwa wa kiharusi, figo kufeli wengi hawakuwa wanajua presha zao. Hawana vipimo.

Unavyotakiwa uwe kuanzia leo: Wewe una kipimo? Unajua namba zako? Ili uweze kudhibiti presha vizuri na kuchukua hatua stahiki mapema inabidi ujue namba zako.

3

Hufanyi Tathmini – Muda mwingi

Athari kubwa: Unajaribu hiki leo na kuacha kesho bila kuona nafuu ya kueleweka. Unagusa tiba hii, unachanganya na ile, unaona inasaidia kidogo lakini baada ya muda presha inapanda tena. Hujui tena nini ufanye na kipi ni sahihi kwako. Huna Uhakika wa chochote ufanyacho.

Ushahidi: Leo presha imepanda, kesho imeshuka. Hujui nini ulifanya jana presha ikashuka ili uendelee nancho au Uache ulichofanya leo.

Unavyotakiwa kuwa: Rekodi na tathmini kila hatua unayoichukuka kudhibiti presha yako. Lengo ni uweze kujua hatua ipi imeweza kudhibiti presha na uendelee nayo kama ilivyo, au hatua ipi imeonesha ufanisi kidogo hivyo uifanyie marekebisho na hatua ipi uachane nayo kwani haina mchango wowote.

Dr. Adinan MD.MSc.Fellow.Fogarty
10+ Miaka ya Uzoefu
Kiongozi na Mtaalamu Mkuu

Dr. Adinan MD, MSc, Fellow Fogarty

Mtafiti wa Magonjwa ya Presha, Kisukari na Moyo | Mbobezi wa Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya

Tangu mwaka 2014, Dr. Adinan amekuwa mstari wa mbele kutafiti na kufundisha wagonjwa kwa mafanikio makubwa katika masuala ya kudhibiti magonjwa sugu ya mfumo wa maisha.

Hivi sasa, anaongoza timu yenye uweledi wa hali ya juu, ari, na kujituma kwa dhati kuhakikisha kila mteja anapata huduma ya karibu na matokeo yanayothibitika.

🔬 Utafiti Uliothibitishwa
🏥 Utaalamu wa Mifumo ya Afya
👥 Timu Iliyojitolea

Kwanini Nimeamua Kusaidia Wagonjwa wa Presha?

Mwaka 2024 nilipokuwa nasoma degree yangu ya Pili, Nilishirikishwa kwenye utafiti wa tathmini kama watu wanaweza kujipima presha kwenye maduka ya dawa Mwanza. Lengo lilikuwa kuboresha ugunduzi wa mapema wa presha ya kupanda ili kuanza matibabu mapema. Alikuja mzee mmoja wa umri wa makamo—ambaye presha yake ilikuwa imepanda kufikia kiwango cha hatari kubwa isiyo ya kawaida ya 215/180 mmHg (Hypertensive Crisis).

💔 “Mwanangu, mbona najisikia vizuri kabisa?”

Nilimmsihi kwa dhati aende hospitali mara moja. Aliniangalia, akatikisa kichwa chake, kisha akatabasamu: “Mwanangu, mbona najisikia vizuri kabisa? Sina dalili yoyote na nina kazi zangu za kufanya.” Aligeuka na kuondoka bila kujua alikuwa anaenda kukutana na mauti.

⚠️ Simu Iliyotikisa Moyo Wangu

Jioni hiyo, simu yangu iliita. Nilipopokea, sauti ya msaidizi wangu wa utafiti ilikuwa ikitetemeka kwa hofu upande wa pili wa simu. Yule mzee alikuwa amepatwa na kiharusi cha kushtukiza (stroke) jana jioni. Alikuwa amelazwa katika wodi ya dharura katika hospitali moja kubwa mjini Mwanza, akiwa hawezi tena kuongezeka wala kujitetea.

🕯️ Muuaji wa Kimya Kimya Asiye na Huruma

Simu hiyo ilinishtua na kuniumiza sana moyoni, lakini pia iliwasha moto mkubwa ndani yangu. Sikuweza kuacha kufikiria jinsi muuaji huyu wa kimya kimya na asiyeonekana anavyonyang’anya familia nguzo zao kwa sababu tu ya ukosefu mdogo sana wa uelewa.

Mzee yule hakukataa matibabu kwa sababu alikuwa mkaidi; alikataa kwa sababu hakuwa anajua. Hakuwa anajua kuwa presha laihitaji kuuma au kutoa dalili ya onyo ili kukupa ulemavu wa kudumu au kuua papo hapo. Hakuwa anajua viwango vyake salama vya presha, hakuwa anajua maana ya kujilinda, wala hakuwa anajua mwamba wa mauti uliokuwa mbele yake.

✊ Kiapo Changu cha Kupambana na Janga Hili

Hapo hapo, niliamua kuwa siwezi kubaki tu pembeni na kuendelea kuhesabu takwimu hizi za majanga ya watu wetu—ilipasa nifanye kitu cha kishujaa kuleta mabadiliko ya kudumu.

Nilipambana na kufanikiwa kupata ufadhili wa utafiti (research grant) mahsusi kwa ajili ya kutatua vikwazo vya ugunduzi wa mapema na udhibiti wa presha ya kupanda. Nilivyoendelea kuchimba kwa undani, ukweli ukawa wazi na wa kuumiza zaidi: ukosefu wa elimu ya afya ni muuaji mkuu nambari moja. Watu hawawezi kudhibiti tatizo ambalo hawalielewi, wala hawawezi kupambana na adui ambaye hawamwoni, haonyeshi dalili, na hasikii maumivu!.

Kuvunja ukimya huo na kuzuia vifo vya kikatili kama vile, tangu 2016 nilianzisha tovuti hii rahisi iliyojitolea kufundisha jamii zetu kuhusu presha na kisukari kwa lugha rahisi wanayoweza kuielewa kikamilifu. Kilichoanza kama kilio na majibu ya dharura ya mchana ule wa huzuni, leo kimekuwa vuguvugu kubwa la kuokoa maisha. Mpaka leo hii tumeshasaidia na kuokoa zaidi ya wagonjwa 1,300.

Sifa za Wateja Wetu

Tunawahudumia Wahitaji Ambao:

Baada ya tathmini yetu ya takwimu, wagonjwa wanaofanikiwa haraka zaidi kwenye PreshaPlan wana tabia hizi:

Wanataka Msaada wa Moja kwa Moja

Umejaribu njia mbalimbali za kudhibiti presha na imeshindikana, ingawa bado unahudhuria kliniki au hospitali mara kwa mara.

Unaamini Ushirikiano na Mtaalamu

Unaamini presha haina tiba ya mkato kwa sasa ila unaweza kuidhibiti, na kwamba ushirikiano wa karibu kati yako na mtaalamu wa afya ndio utakaofanikisha udhibiti huo.

Utayari wa Kuchukua Hatua

Uko tayari kuchukua hatua stahiki kwa wakati kulingana na ushauri wa wataalamu wetu, ikiwemo mabadiliko ya vyakula, mazoezi, na kutathmini afya yako.

Utayari wa Kutumia Zana Zetu

Uko tayari kujipima na kufuatilia majibu yako. Tutakupatia Kipimo cha Dijitali cha Presha, Kitabu cha Mwongozo wa Vyakula na Kuepuka Madhara, pamoja na KIPA App kwa ajili ya kurekodi vipimo na kupata elimu sahihi.

Matokeo Yaliyothibitishwa

Mafanikio ya Wateja Wetu Kufikia Sasa

0+ Tuliowasaidia
0+ Waliodhibiti
0% Mafanikio
Tupo Pamoja Nawe

Namna Tunavyokusaidia Kudhibiti Presha!

Kuwa na amani:

AFYATech inakuletea huduma ya PreshaPlan – mpango wa kitaalamu unaokusaidia kudhibiti shinikizo la damu kwa njia salama, bila hofu, na bila kubaki peke yako. Huduma hii imesaidia Watanzania wengi tangu mwaka 2016 kupata utulivu na amani ya afya.

01

Kujisajili na Kufanyiwa Tathmini

Tunapitia taarifa zako za kiafya kujua kiwango na aina ya presha unayopata. Baada ya hapo tunakupendekezea mpango unaokufaa.

02

Mpango wa Kudhibiti Presha

Tunakuandalia mpango wa vyakula, mazoezi, na mtindo wa maisha unaokufaa. Unapata ushauri wa moja kwa moja kupitia AfyaPlan App kila wiki.

03

Ufuatiliaji na Tathmini

Tunatathmini maendeleo yako kila wiki kuhakikisha afya yako inaimarika na presha yako inakaa kwenye kiwango salama.

SULUHU YAKO KAMILI NA YA KITAALAMU

Nyenzo 3 Tunazozitumia Kukusaidia Kudhibiti Presha Nyumbani

Hustahili kuishi kwa hofu au kucheza bahati nasibu na afya yako. Tumeunganisha teknolojia na elimu bora ya tiba ili kukupa ulinzi usiotikisika dhidi ya kiharusi na kufeli kwa viungo.

Nyenzo Na. 1

Kipimo cha Presha cha Digitali Kinachotambulika Kimataifa

Kipimo hiki cha kisasa kabisa kina viwango vya kimataifa vya usahihi (ISO & CE Certified). Kinakupa majibu ya haraka na sahihi ya sekunde chache ukiwa nyumbani kwako—bila haja ya kupanga foleni ndefu au kulipia gharama za hospitali kila siku. Ni rahisi kutumia hata kwa wazee!

  • ⚡ Majibu ya Uhakika & Ya Haraka (Instant Accuracy)
  • 🔋 Mfumo wa Kidigitali Rahisi Kutumia Mwenyewe
  • 🛡️ Kinakutahadharisha Hali ya Hatari Mapema Sasa
Nyenzo Na. 2

Kitabu Mwongozo wa Vyakula vya Kudhibiti Presha (PDF)

Acha kuacha kula vyakula unavyovipenda kwa hofu isiyo na msingi! Mwongozo huu wa kitiba unakufundisha siri za kisayansi za mchanganyiko wa vyakula vya asili vinavyoshusha na kuweka presha kwenye kiwango salama kwa kufuata ratiba sahihi na yenye ladha nzuri.

  • 🥗 Ratiba ya Mlo wa Wiki Nzima ya Vyakula vya Kitanzania
  • ❌ Vyakula Vinavyoshusha Presha & Vinavyopaswa Kuepukwa
  • 📖 Mfumo wa PDF Utakaosoma Kwenye Simu Yako Wakati Wowote
Nyenzo Na. 3

Mobile App ya KIPA (Msaidizi Wako wa Kila Siku)

KIPA App ni kiganja chako cha afya! Inakusaidia kutunza na kufuatilia takwimu za presha yako kila siku, kushiriki kwenye darasa la afya na elimu endelevu, pamoja na kupata fursa ya kujadiliana na kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa Dr. Adinan na wataalamu wenzake.

  • 📱 Rekodi na Fuatilia Trend ya Presha Yako Kila Siku
  • 🎓 Mfumo wa Madarasa & Masomo ya Afya Endelevu
  • 👨‍⚕️ Mawasiliano na Majadiliano ya Moja kwa Moja na Daktari
Ratiba ya Mafanikio

Wiki 12 Unapokuwa kwenye PreshaPlan

Hatua kwa hatua kuelekea afya bora na utulivu wa presha yako

WIKI YA 1: Kuanza Safari Yako
Siku ya 1 🩺

Medical Doctor – Tathmini ya Awali

Tathmini ya awali, uchambuzi wa historia ya afya, na mikakati ya awali ya tiba na ufuatiliaji.

Siku ya 2 🍎

Lishe & Vyakula

Uchambuzi wa lishe na mapendekezo ya vyakula sahihi vinavyosaidia kupunguza na kudhibiti presha kulingana na vyakula unavyopendelea na vinavyopatikana ulipo.

Siku ya 3 🧘🏽‍♂️

Mazoezi Salama

Mwongozo wa mazoezi salama yaliyopimwa maalum kusaidia kushusha shinikizo la damu.

Siku ya 4 🧠

Mshauri/Mwanasaikolojia

Mbinu za kisaikolojia na udhibiti wa msongo wa mawazo (stress) unaosababisha presha kupanda.

Siku ya 5 👥

Kukuhakikishia Unaweza!

Kujifunza ushuhuda na mbinu za vitendo kutoka kwa waliofanikiwa kudhibiti presha zao kikamilifu.

Wiki 2 – 12

Vikao vya Ufuatiliaji Kila Wiki

Ufuatiliaji wa karibu na tathmini ya matokeo yako unaofanywa na Daktari pamoja na wataalamu wengine wa afya mara kwa mara inapohitajika hadi kuhakikisha afya yako inatengemaa kikamilifu.

Ushuhuda Halisi

Wanavyosema Waliojiunga!

Tazama jinsi PreshaPlan inavyobadilisha maisha ya watu kote nchini.

⭐⭐⭐⭐⭐

“Nimependa kila kitu kwenye hii PreshaPlan. Wataalamu ni wakarimu sana! Nampenda sana Psychologist wenu.”

JJ
Jane John 📍 Mwanza
⭐⭐⭐⭐⭐

“Nilichopenda kwenye AfyaPlan ni mimi kushauriana na wataalamu wa afya hivyo kushiriki moja kwa moja. Pia timu yenu ina wataalamu wote wanaotakiwa!”

JK
Julia Keys 📍 Moshi
⭐⭐⭐⭐⭐

“Nimefanikiwa kudhibiti presha. Nilikuwa nahofu ya kupata kiharusi. Sasa naweza kufahamu hali yangu kwa uhakika.”

UM
Ussy Mzee 📍 Kilimanjaro
⭐⭐⭐⭐⭐

“Mwanzo nilikuwa na hofu kwamba inafanyika kwenye mtandao (online). Lakini nimejifunza kwamba inanipa uhuru na najidiliana na madaktari kwa wakati muafaka bila kuathiri ratiba zangu.”

MB
Morsa Bilal 📍 Zanzibar
⭐⭐⭐⭐⭐

“Nilichofurahia ni kurudia kula vyakula nilivyokuwa navipenda kwa mpangilio bora bila kuathiri presha yangu sana. Nilikuwa nakula ndizi changa tuu!”

SH
Salim Hashim 📍 Dar es Salaam
⭐⭐⭐⭐⭐

“Vitabu vyenu vizuri na vinaelimisha sana. Pia elimu itolewayo huku ni nzuri na inavutia kwakweli.”

HM
Honest Moshi 📍 Arusha

Epuka Madhara: Changua Mpango wako Sasa.

Chagua mpango unaokufaa leo tuanze safari ya kurejesha amani yako!

Digital Learning & Tracking

Kitabu na KIPA App

Tumia App ya KIPA na Kitabu kuendelea kujifunza, kufuatilia vipimio vyako kiotomatiki na kupima ufanisi wa matibabu yako kwa urahisi.

  • ✅ Kitabu cha Presha na Kisukari
  • ✅ KIPA Mobile App Access (Mafunzo & Mazoezi)
  • ✅ Kufuatilia Vipimio (Presha, Sukari & Uzito)
  • ✅ Kupima Ufanisi wa Matibabu & Ripoti
  • ✅ Elimu ya Lishe na Mfumo wa Maisha
TSh. 75,000/= TSh. 39,000/=
Pata Kitabu na KIPA App (TSh 39,000/=)
Package Kamili

Full PreshaPlan + Vifaa Vyote

Pata kila kitu unachohitaji kuanza safari yako ya kudhibiti presha na kisukari kikamilifu bila kukosa kifaa chochote.

  • ✅ Kipimo cha Presha cha Digitali
  • ✅ Kipimo cha Sukari
  • ✅ Kipimo cha Uzito
  • ✅ Kitabu cha Presha na Kisukari
  • ✅ KIPA Mobile App + Ufuatiliaji wa Daktari
TSh. 280,000/=
Nataka Kujiunga Full PreshaPlan
🔥 Nafasi 5 Tu Zimebaki
Ofa inaisha baada ya Saa: 48:00:00
Chagua Kifurushi Hapo Juu ↑

🔒 Huduma ya Uhakika na Ufuatiliaji wa Karibu

Scroll to Top