Kuwa na Amani: Pata msaada wa Ki Afya Popote Ulipo na Wakati Wowote
Tatizo: Watu wengi wanaogopa kwenda hospitali au kuomba msaada wa kitaalamu wanapokuwa wagonjwa, badala yake hutegemea ushauri kutoka kwa marafiki, jamaa au mtandaoni.
Hali hii inaweza kupelekea kupata ushauri usio sahihi na mbinu zisizofaa, kama vile mmoja wa washiriki wetu wa AfyaPlan aliyedhani ana saratani kwa sababu tu alikuwa anatoka damu akijisaidia.
Wagonjwa wengi wanapenda kupata majibu ya haraka kwa maswali yao ya kiafya mtandaoni, lakini wanapoambiwa kuna gharama, wanaanza kuwa na mashaka kuhusu huduma hiyo.
Kwa mfano, mtu anapouliza maswali na kupata majibu yenye manufaa kutoka kwa wataalamu wetu wa AfyaPlan, huendelea kuuliza zaidi na kufurahia majibu.
Lakini, anaposema kuhusu gharama, mara nyingi hujawa na wasiwasi na hofu ya kutapeliwa, na hivyo anaanza kutafuta majibu kwenye mitandao mingine ambayo yanaweza kuwa si ya kweli au yenye madhara.
AfyaPlan inakuletea fursa ya kupata huduma bora za afya mtandaoni, huku ukiwa na uhakika wa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa madaktari waliothibitishwa na wazoefu.
Gharama unazolipa ni kwa ajili ya huduma bora na ushauri sahihi, ambavyo vitakusaidia kuepuka madhara na gharama zisizo za lazima za matibabu yasiyo sahihi.
Mfano: Mshiriki mwingine karibu apate kiharusi baada ya kufuata ushauri wa mtu asiyejulikana kutumia dawa za mitishamba badala ya dawa za shinikizo la damu alizopaswa kutumia. Hii ni hatari ya kuamini habari zisizo sahihi.
Faida: Ukiwa na AfyaPlan, utapata ushauri sahihi kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu, hivyo kupunguza hofu na kukusaidia kuchukua hatua bora za kiafya. Kwa mfano, utaepuka gharama zisizo za lazima kwa kutumia matibabu sahihi mara moja, na kuokoa muda muhimu wa kupata nafuu.
Kwa Nini Unahitaji AfyaPlan:
- Kama bado hujakwenda hospitali: Unahitaji AfyaPlan ili kuhakikisha unapata ushauri wa kitaalamu, siyo wa kubahatisha kutoka kwa watu wasio na utaalamu. Kwa kujiunga, utaishi bila hofu, ukiwa na uhakika wa usimamizi bora wa afya yako kutoka kwa wataalamu.
- Umeanza matibabu hospitali: Tutakuwa nawe popote wakati wowote unapokuwa nje ya hospitali. Lengo letu ni kuendeleza matibabu yako na kuhakikisha kwamba unaendelea kufurahia maisha kwa kuwa na afya bora. Hivyo tutakupatia AfyaPlans App kuhakikisha unafuatilia afya yako kwa ukaribu zaidi hivyo kukuwezesha wewe na daktari wako kufanya maamuzi stahili kwa wakati.
- Unapenda kujielimisha zaidi: Jiunge sasa na ufurahie amani ya akili na afya bora!