Kuelewa mzunguko wako wa hedhi ni mojawapo ya mambo muhimu zaidi unayoweza kufanya kwa ajili ya afya yako ya uzazi. Lakini kwa wengi, kuna sintofahamu kubwa inayozunguka hasa neno moja: siku za hatari.
Hivi karibuni, mgonjwa mmoja alinieleza akiwa na huzuni kubwa:
“Nilidhani nipo kwenye siku salama, kumbe nilikuwa kwenye siku za hatari. Nilipata ujauzito bila kupanga.”
Kisa chake kinafanana na cha wanawake na wanaume wengi – aidha wanashindwa kupata ujauzito kwa sababu hawajui lini hasa ni siku za kupata mimba, au wanapata ujauzito bila kutarajia kwa sababu ya taarifa zisizo sahihi.
Upo Tayari Kuacha Kubahatisha?
Jiunge na zaidi ya wanufaika 500 nchini Tanzania wanaotumia AfyaPlan kupanga familia zao kwa uhakika na kujiamini. Weka maisha yako mikononi mwako.
Lakini kabla hatujazama kwenye mahesabu, ni muhimu kuelewa mtego mkubwa unaowafanya wengi wakosee na kuingia kwenye hali kama hii.
Mtego wa Kalenda: Kwa Nini Njia za Kawaida Zinatuangusha?
Wengi wetu tumefundishwa kukadiria kwa kutumia kalenda ya kawaida, lakini ukweli ni kwamba njia hii imejaa changamoto zinazoweza kubadili maisha yako:
- DHANA POTOFU YA SIKU 28: Je, unafahamu kuwa mzunguko wa “siku 28” ni wastani tu? Wanawake wengi hawana mzunguko huu. Mzunguko wako unaweza kuwa wa siku 24, 35, au kubadilika kila mwezi. Kutegemea mahesabu ya “kitabuni” ni kama kuvaa kiatu cha mtu mwingine na kutegemea kikutoshe.
- ADUI ANAYEITWA MAISHA: Mzunguko wako si mashine. Wiki moja tu yenye msongo wa mawazo (stress), mabadiliko ya lishe, safari, au mazoezi makali inaweza kuchelewesha au kuwahiisha siku yako ya ovulation bila wewe kujua. Unapokadiria, unakuwa hujazingatia uhalisia wa maisha yako.
- GHARAMA YA KUBAHATISHA: Kukosea kwa siku moja tu kunaweza kumaanisha kupata ujauzito usiotarajiwa au kukosa dirisha muhimu la kupata mimba ambalo umelisubiri kwa muda mrefu. Je, upo tayari kuweka mustakabali wako kwenye mahesabu ya kubahatisha?
Hofu na wasiwasi unaotokana na kutokuwa na uhakika ndiyo sababu hasa teknolojia imeleta suluhisho bora zaidi.
AfyaPlan: Suluhisho Lako la Uhakika na Amani ya Akili
Fikiria kama ungekuwa na kalenda yenye akili mfukoni mwako. Kalenda isiyotegemea wastani wa kubahatisha bali inayojifunza na kuelewa mzunguko wako wa kipekee. Hiyo ndiyo Kalenda ya uzazi wa mpango ya AfyaPlan.
App hii inaondoa kubahatisha kwa:
- Kukokotoa Kiotomatiki: Inajifunza urefu wa mzunguko wako na kutabiri kwa usahihi zaidi dirisha lako la uzazi (siku za hatari).
- Kukupa Amani ya Moyo: Ondoa wasiwasi wa “Je, leo niko salama?”. Pata majibu ya uhakika kwa kugusa tu simu yako.
- Kukukumbusha: Inakutumia vikumbusho muhimu kuhusu hedhi inayokaribia na siku zako za kupata mimba ili usisahau.
Jinsi Unavyoweza Kuhesabu Siku za Kupata Mimba (Mfano wa Mzunguko wa Siku 28)
Ili upate uelewa wa kimsingi, hivi ndivyo wataalamu wanavyokadiria siku za hatari kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28 usiobadilika:
Dirisha la Uzazi (Fertile Window) ni takriban siku sita (6) katika kila mwezi. Linategemea uhai wa mbegu ya kiume (hadi siku 5) na uhai wa yai (saa 24).
- Hatua ya 1: Jua Siku Yako ya Kwanza. Weka alama kwenye kalenda siku unayoanza kupata hedhi. Hiyo ndiyo Siku ya 1 ya mzunguko wako.
- Hatua ya 2: Tafuta Siku ya yai kupevuka (kimombo, Ovulation). Katika mzunguko wa siku 28, ovulation hutokea katikati, yaani siku ya 14. (Hesabu siku 14 kutoka Siku ya 1).
- Hatua ya 3: Tambua Dirisha Kamili. Hesabu siku tano (5) nyuma kutoka siku ya ovulation (Siku ya 14). Hii inamaanisha dirisha lako la hatari linaanza Siku ya 9 na kuishia Siku ya 14. Hizo ndizo siku zako za hatari zaidi.
Mwili wako pia hutoa ishara kama mabadiliko ya ute ukeni (unakuwa mweupe na wa kunyumbulika) au maumivu mepesi ya tumbo.
Usiharibu Amani Yako: Usikosee Makadirio
Kama ulivyoona, mahesabu ya kalenda yanategemea mzunguko wako uwe umetulia kama saa, jambo ambalo ni nadra kwa wengi.
Badala ya kuishi kwa wasiwasi na kubahatisha, tumia teknolojia iliyothibitishwa kukuongoza.
AfyaPlan haichukui nafasi ya ushauri wa daktari, bali inakupa zana ya kukusaidia wewe na daktari wako kufanya maamuzi sahihi.
“Tangu nianze kutumia AfyaPlan, nina amani ya akili. Hakuna tena wasiwasi kila mwezi.” – Mtumiaji wa AfyaPlan
Anza Kujiamini Leo!
