- Tonsils ni nini?
Tonsils ni tezi za kinga zinazopatikana nyuma ya koo pande zote mbili. Kazi yake ni kusaidia mwili kupambana na maambukizi kwa kunasa na kuharibu vijidudu vinavyoingia kupitia mdomoni na puani. Ingawa ni sehemu muhimu ya mfumo wa kinga, wakati mwingine tonsils zinaweza kuvimba au kuambukizwa na kusababisha matatizo ya kiafya.
- Dalili za Tonsils (Tonsillitis)
Dalili zinazoweza kujitokeza ni pamoja na:
- Maumivu ya koo
- Ugumu au maumivu wakati wa kumeza
- Homa
- Kuvimba kwa tonsils na kuwa nyekundu
- Madoa meupe au usaha kwenye tonsils
- Harufu mbaya ya mdomo
- Kuvimba tezi za shingoni
- Kukoroma au kushindwa kupumua vizuri wakati wa kulala, hasa kwa watoto
- Njia za Utambuzi na Matibabu
Utambuzi
- Kuchukua historia ya ugonjwa kutoka kwa mgonjwa.
- Uchunguzi wa koo, pua na masikio.
- Vipimo vya maabara pale inapohitajika, kama vile kipimo cha maambukizi ya bakteria.
Matibabu
- Dawa za kupunguza maumivu na homa.
- Kunywa maji ya kutosha na kupumzika.
- Antibiotiki iwapo maambukizi yamesababishwa na bakteria.
- Upasuaji wa kuondoa tonsils (tonsillectomy) kwa wagonjwa wenye maambukizi ya mara kwa mara au wanaopata matatizo ya kupumua kutokana na tonsils kubwa.
Hitimisho
Matibabu ya mapema husaidia kuzuia madhara na kuboresha afya ya mgonjwa.
Wasiliana nasi kwa msaada zaidi.
Dr Kenny Mlay(MD, MMED, Head & Neck Surgery) +2557 13137433