Taarifa ya Muhimu

Kwa nini ni vigumu kujua kama una presha?

Presha mara nyingi haina dalili hadi wakati madhara yanapoanza (kiharusi, moyo kushindwa, nk.).

Kuamini hisia pekee si salama — kupima ndio njia sahihi. Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza umuhimu wa utambuzi wa mapema ili kuzuia madhara makubwa.
Mwongozo wa Vitendo

Jinsi Sahihi ya Kubaini Kama Una Presha

Hatua 7 za kufanya nyumbani zilizothibitishwa kitaalamu:

1
Pumzika kabla ya kupima: Kaa kimya kwa dakika 5, ukiwa umeegemea vizuri.
2
Kaa kwa mkao sahihi: Weka miguu chini ardhini (bila kukatiza miguu) na mgongo ukiwa umeegemea.
3
Mikono sawa na moyo: Weka mkono juu ya meza; cuff iwe juu kidogo ya kiwiko.
4
Epuka vitu vinavyostimulate presha: Usile, unywe (chai/kahawa), au kufanya mazoezi dakika 30 kabla.
5
Utulivu wa mwili: Usitingishe au kukunja miguu wakati wa kipimo, na wala usizungumze.
6
Chukua wastani: Fanya vipimo mara 2–3, ukisubiri dakika 1–2 kati ya kila kipimo, kisha chukua wastani.
7
Tengeneza rekodi: Rekodi namba na muda kila siku kwa wiki 1 ili kupata mwelekeo sahihi.

Ulinganisho: Mkono wa Juu vs. Kiganjani

Kipimo cha Mkono wa Juu (Arm)

Chaguo la kwanza la madaktari (AHA). Ni sahihi zaidi kwa matumizi ya nyumbani.

Nani HAFFAI kutumia:

  • Watu wenye majeraha makubwa kwenye mkono wa juu.
  • Watu waliofanyiwa upasuaji wa kuondoa nodi za limfu (lymph nodes) upande huo.

Kipimo cha Kiganjani (Wrist)

Rahisi kubeba, lkn linahitaji usahihi wa mkao (usawa wa moyo).

Nani HAFFAI kutumia:

  • Wagonjwa wa Kisukari: Mishipa yao ni migumu (stiff), ikileta matokeo yasiyo sahihi.
  • Wazee: Mishipa ya kiganjani inakuwa dhaifu kwa umri.
  • Wavuta Sigara: Uvutaji huathiri mishipa midogo ya mbali na moyo.
  • Wenye matatizo ya moyo (Arrhythmia): Mdundo usio sawa huathiri usomaji.
Omron BP Machine

Omron M2/M3

Usahihi wa hali ya juu na teknolojia ya IntelliSense. Bora kwa familia.

Nunua Omron Sasa
Arm Monitor

Arm Monitor Standard

Chaguo la uhakika kwa ajili ya matumizi ya kila siku ya nyumbani.

Nunua Kipimo cha Mkono
Wrist Monitor

Wrist Monitor

Teknolojia ya kisasa kwa wasafiri na matumizi ya haraka popote.

Nunua Kipimo cha Kiganja

Unapopata Matokeo Gani — Nini Ufanye?

Kipimo (mmHg)HaliHatua za Kuchukua
Chini ya 120/80KawaidaEndelea na mtindo mzuri wa maisha; pima mara kwa mara.
120–129 / <80Imepanda KidogoFanya mabadiliko ya mlo na mazoezi; fuatilia kwa karibu.
130–139 / 80–89Presha Daraja la 1Ongea na mtoa huduma; unahitaji mabadiliko ya maisha na pengine dawa.
≥ 140/90Presha KubwaTafuta ushauri wa daktari mara moja — inaweza kuhitaji tiba au marekebisho ya dawa.

Mambo ya Kufanya Sasa hivi

🛒

1. Nunua Mashine Halisi

Kagua au nunua mashine ya kupima presha ya kiganjani/mkononi yenye memory na offa ya kipekee.

Nunua Mashine Yako
📋

2. Jiunge na AFYAPlan

Hifadhi matokeo yako kila siku, pata ushauri wa lishe, na ufuatiliaji wa karibu wa daktari.

Jiunge na Programu

💡 Faida ya Kupima Presha Nyumbani

Kupima nyumbani husaidia kugundua presha ya ‘White Coat’ (inapanda vibaya tu ukiwa kliniki) na kubaini mabadiliko ya kila siku — hivyo kurahisisha maamuzi ya daktari juu ya tiba sahihi kwako.

⚠️ Je, vipimo vinaweza kuwa sahihi kila wakati?

Hapana. Sababu zinazoweza kuleta matokeo yasiyo sahihi ni pamoja na:

  • Cuff isiyofaa au kufungwa vibaya mkononi.
  • Mkao usiofaa wakati wa kupima.
  • Kunywa kahawa/chai au kufanya mazoezi muda mfupi kabla ya kipimo.

Usipime Presha na Vifaa Feki!

AFYATech inakupa mashine halisi (Original) zenye warranty. Tunafanya delivery Tanzania nzima.

PATA KIPIMO CHAKO SASA
Scroll to Top