Maji ya kunywa yanaboresha vipi afya yako?
Siku zote tumesikia kwamba tunapaswa kunywa maji mengi kwa siku. Lakini je! kwa nini? Na ni kiasi gani cha maji ambayo mtu mzima anapaswa kunywa kwa siku?
Kwa kuanza, maji ni muhimu sana kwa afya yetu. Maji yanasaidia kuondoa sumu mwilini, kusaidia mmeng’enyo wa chakula, na kuboresha afya ya ngozi, husaidia kuepuka presha ya kushuka na afya kwa ujumla.
Kwa hivyo, ni muhimu sana kunywa maji ya kutosha kila siku.
Nini huathiri kiasi cha maji ninachotakiwa kunywa kwa siku?
Kwa kawaida, wataalam wanapendekeza kwamba mtu mzima anapaswa kunywa kati ya lita mbili hadi tatu za maji kwa siku.
Hatahivyo, kiwango kinaweza kutofautiana kulingana na uzito, hali yako ya kiafya, kiwango chako cha shughuli za kimwili kama mazoezi, na hali ya hewa.
- Mazoezi: Kwa mfano, ikiwa unafanya mazoezi mengi au
- Joto: unaishi katika hali ya hewa ya joto, unaweza kuhitaji kunywa maji zaidi ili kudumisha kiwango chako cha unyevu.
- Ugonjwa: Vivyo hivyo, ikiwa una matatizo ya afya kama vile figo au moyo, unapaswa kuzungumza na daktari wako kuhusu kiasi cha maji unachopaswa kunywa kwa siku.
- Aina ya vyakula unavyokula: Ni muhimu kutambua kwamba pia huwa tunapata maji kutoka kwenye vyakula tunavyokula kama vile mtori, uji (uji ni kinywaji au chakula?), vinywaji vingine pia, kama vile chai, kahawa, na juisi.
Namna ya kufahamu kiasi sahihi cha maji ya kunywa kwa siku
Kufahamu kiasi sahihi cha maji ya kunywa ni muhimu kuhakikisha kuwa unakunywa maji ya kutosha kila siku ili kudumisha afya yako na ustawi.
Kama ilivyopendekezwa hapo awali, kunywa kati ya lita mbili hadi tatu za maji kwa siku ni kiasi cha wastani ambacho mtu mzima anapaswa kunywa.
Tunza afya yako na kumbuka kunywa maji ya kutosha kila siku!
Kama tulivyoona hapo juu pia, kiwango cha maji ya kunywa huweza kubadilika kutokana na hali fulani.
Fuata hatua hizi kufahamu kiwango cha maji ya kunywa unachohitaji kwa siku.
Hatua ya 1: Pima uzito wako kwenye kilo
Mtu mwenye kilo nyingi huitaji maji kiasi kikubwa kuliko mwenye kilo ndogo.
Kwa mfano, mtu mwenye kilo 80 anahitaji kiasi cha maji zaidi ya mtu mwenye kilo 50.
Hatua ya 2: Gawanya uzito kwa 30
Gawanya uzito wako kwa 30. Jibu utakalopata ni kiasi cha lita za maji unazopaswa kunywa kwa siku.
Kwa hivyo, ikiwa una uzito wa kilo 30 kwa mfano, unapaswa kunywa lita moja ya maji kwa siku, ambapo ikiwa una kilo 75, unapaswa kunywa lita 2.5 (lita 2 na nusu) za maji kwa siku.
Hatua ya 3: Ongeza maji zaidi kama unajishughulisha na shughuli zinazotumia nguvu au unafanya mazoezi
Ikiwa unafanya mazoezi, unaweza kupoteza maji mengi kwa jasho. Ongeza lita 0.35 (350 ml) kwa takwimu kwa kila nusu saa unayofanya mazoezi.
Kwa hivyo, ikiwa unafanya mazoezi kwa saa moja kila siku, ongeza lita 0.7 (700 ml) za maji kwa mahitaji yako ya kila siku.
Nambari uliyobaki nayo ni idadi ya lita za maji ambazo mwili wako unahitaji kila siku.
Je, ninywe maji ya kunywa kiasi gani? Kumbuka kwamba chakula kina maji pia
Kwa bahati nzuri, sio lazima kunywa maji hayo yote kwa sababu utapata kiasi kingine cha maji kutoka kwenye chakula chako. Inakadiriwa kwamba mtu hupata takribani 20 – 25% ya maji unayohitaji kwa siku kutoka kwenye chakula.
Kwahiyo utapunguza kiasi cha maji ya kunywa kutoka kwenye mahesabu uliyofanya hapo juu kulingana na kiwango cha maji unayoyapata kwenye chakula.
Kwamfano wewe una kilo 60 na unakunywa unakunywa chai nusu Lita kwa siku, hali ya hewa ni ya kawaida na hufanyi mazoezi, utahitaji kunywa Lita 1.5 ya maji.
Kwamba, wewe unahitaji 60/30, Lita 2 kwa siku. Unatoa nusu Lita ya chai na hivyo unabaki kuhitaji Lita 1.5 ya maji ya kunywa.
Hitimisho kuhusu kiwango cha maji ya kunywa kwa siku
Hata katika maji ya kunywa, bado tunabaki na msingi wetu ule ule kwamba kila mtu ni tofauti na mwenzake na mazingira yanaweza kuwa tofauti pia.
Hivyo, kiwango cha maji kinaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu kulingana na uzito, shughuli za mwili, hali ya hewa na afya ya mtu.
Makala hii ingawa haijaweza kukadiria kiwango cha maji kwa kuzingatia hali zote zinazoweza kutokea kwenye mazingira na mtu tofauti tofauti, inakuwezesha kufahamu kiwango cha mahitaji yako ya maji kwa angalau 95% – hivyo itumie.
Ukiwa na wasiwasi wasiwasi wowote kuhusu kiasi cha maji ya kunywa unachohitaji, usisite kuwasiliana na tabibu wako au kutuuliza.
SAIDIA WENGINE
- Tutafurahi kusikia maswali au maoni yako kuhusu makala haya. Tafadhali tuandikie hapo chini.
- Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu.