-
DAYS
-
HOURS
-
MINUTES
-
SECONDS

Ongea na Daktari Kwa Nafasi!

Mambo 3 Muhimu Kuhusu Dawa za Presha

Je, nianze kutumia dawa za Presha?

Dawa za presha ni muhimu sana katika matibabu ya kudhibiti shinikizo la damu. Ikiwa umeshindwa kudhibiti presha kwa kubadili mtindo wa maisha kama vile vyakula, au kufanya mazoezi basi unahitaji kutumia dawa za presha.

Kuna mambo matatu muhimu ambayo ni lazima uyazingatie unapotumia dawa hizi:

1. Dawa za presha zinadhibiti presha

Dawa za presha zina jukumu la kudhibiti shinikizo la damu. Zinawezesha kurekebisha kiwango cha presha mwilini na kuhakikisha kuwa mishipa ya damu inabaki katika hali ya kawaida.

Hii ni muhimu sana kwa afya yako na inaweza kuzuia madhara makubwa kama vile kiharusi, shambulio la moyo, au matatizo ya figo.

2. Dawa za presha ziko za aina nyingi na zinafanya kazi kwa namna tofauti

Dawa za presha zinapatikana katika aina tofauti na kila aina inafanya kazi kwa njia tofauti. Hii inamaanisha kuwa unaweza kubadilisha dawa unayotumia ikiwa inaleta madhara au maudhi.

Kwa mfano, kichwa huwauma baadhi ya watu wanaotumia nifedipine au wengine hupata kikohozi kikavu wanapotumia captopril.

Ukiona huweza kuvumilia maudhi haya wasiliana na daktari wako ili abadilishe dawa.

3. Usiache Bila Ushauri wa Daktari

Matumizi ya dawa ya presha yanafanana na matumizi ya tochi kwenye giza. Tochi huleta mwanga, tochi haiondoi giza. Unapozima tochi hutoona. Hivyo hivyo, dawa za presha hudhibiti presha hivyo usiache bila kushauriana na daktari

Unaweza Kuepuka Kiharusi

Jifunze Kwa Wataalamu Kupitia Jukwaa Letu

Aina ya Dawa za Kushusha Presha

Kuna makundi kadhaa ya dawa zinazotumiwa kutibu shinikizo la damu. Hapa ni baadhi ya makundi hayo:

Kuna makundi mengine ya dawa za presha kama vile vizuizi vya chaneli za kalsiamu, vizuia beta, vizuizi vya renin, vizuizi vya alpha, dawa za kutanua mishipa, dawa za kukinzana na aldosterone, na dawa za mchanganyiko.

Kila kundi lina njia yake ya kufanya kazi na inaweza kuwa na madhara na maudhi tofauti. Ni muhimu kushauriana na daktari wako ili kupata dawa inayokidhi mahitaji yako na inayokufaa zaidi.

1. Dawa za presha za kupunguza kiwango cha maji mwilini

Diuretics ni dawa ambazo hufanya kazi kwa kuongeza mkojo. Hii husaidia kupunguza kiwango cha maji katika mishipa ya damu na kusababisha kupungua kwa shinikizo la damu.

Baadhi ya maudhi ya kawaida ya diuretics ni pamoja na kukojoa mara kwa mara na kuathiriwa kwa uwiano wa electrolyte.

2. Dawa za presha za kuzuia mishipa ya damu kusinyaa – Vizuizi vya ACE

Dawa hizi za presha huzuia mishipa ya damu kukakamaa. Kwa kuzuia mishipa kukakamaa, presha ya damu inapungua. Baadhi ya maudhi ya kawaida ya vizuizi vya ACE ni pamoja na kikohozi. Mifano ya dawa hizi ni captropril na lisinopril.

3. Dawa za presha za kufanya mishipa kutanuka – (CaBlockers)

Dawa za kupunguza misuli ya mishipa ya damu kukakamaa – Vizuizi vya chaneli za kalsiamu hufanya kazi kwa kulegeza misuli kwenye mishipa ya damu. Kulegeza misuli kwenye mishipa ya damu husaidia mishipa ya damu kupanuka na hivyo kupunguza shinikizo la damu.

Baadhi ya maudhi ya kawaida ya Vizuizi vya njia za kalsiamu ni kuvimbiwa au kuvimba kwa vifundo vya miguu. Mfano wa dawa hizi ni Amlodipine na Nifedipine 

Dawa za kutanua mishipa: Dawa hizi hufanya kazi kwa kutanua mishipa ya damu, hivyo kupunguza shinikizo la damu. Mifano ya vasodilators ni pamoja na hydralazine (Apresoline) na minoxidil (Loniten).

Maudhi ya kawaida ya vasodilators ni pamoja na maumivu ya kichwa, shinikizo la chini la damu, na mapigo ya moyo. Wanaweza pia kusababisha uhifadhi wa maji, ambayo inaweza kusababisha uvimbe kwenye miguu, au mikono.

4. Dawa za presha za kupunguza mapigo ya moyo

Dawa hizi hufanya kazi kwakupunguza kiwango cha mapigo ya moyo na shinikizo la damu. Baadhi ya maudhi ya kawaida ya Vizuizi vya Beta vinaweza kusababisha uchovu au kutokuwa na nguvu.

5. Dawa za presha mchanganyiko

Hizi ni dawa zinazochanganywa katika kidonge kimoja. Aina mbili au zaidi za dawa za shinikizo la damu huweza kuchanganywa na kuwekwa katika kidonge kimoja.

Mambo 3 ya kuzingatia unapotumia dawa za presha

  1. Utaratibu wa matumizi ya dawa za presha ni muhimu sana. Ni vyema kufuata maagizo ya mtoa huduma wako wa afya kuhusu matumizi ya dawa hizo. Hii inaweza kujumuisha kutumia dawa kwa wakati maalum kila siku, pamoja na au bila chakula, au kuepuka vyakula au vinywaji fulani ambavyo vinaweza kuathiri ufanisi wa dawa.

  2. Ni muhimu pia kuendelea kutumia dawa hata kama unajisikia vizuri au huna dalili zozote. Kuruka dozi au kuacha dawa kunaweza kuongeza shinikizo la damu na kuongeza hatari ya athari za ugonjwa wa presha. Hivyo, ni vyema kuwa mwangalifu na kufuata maagizo yote ya daktari wako. Wakati mwingine, daktari wako anaweza kukushauri kubadilisha dawa au kurekebisha dozi yako ili kuhakikisha kuwa unapata matokeo bora. Ni muhimu kuwasiliana na mtoa huduma wako wa afya ikiwa una matatizo yoyote, madhara au maudhi unapotumia dawa za presha. Daktari wako atakuwa na ujuzi na uzoefu wa kukushauri vizuri zaidi.

  3. Fuatilia presha yako wakati wote. Unatumia dawa za kushusha presha. Hutaki presha yako ishuke sana kwani huleta madhara ikiwemo kifo. Pia ungependa kuhakikisha ufanisi wa tiba. Hivyo ni LAZIMA kipimo cha presha kiwe karibu nawe wakati wote. Bonyeza HAPA kupata Kipimo cha presha leo kwa bie ya offer!

Madhara ya Dawa za Presha

Kama ilivyo kwa dawa zote, dawa za presha zinaweza kuwa na athari na maudhi madogo. Ni muhimu kuelewa maudhi haya ili uweze kuchukua hatua stahiki.

Scroll to Top