Vidonda Vya Miguuni Kwa Mgonjwa Kisukari : Fahamu Chanzo, Athari, Tiba na Kinga

Vidonda Vya Miguu na Namna Ya Kuviepuka

Vidonda vya kisukari vimekuwa sababu inayoongoza kwa kusababisha ulemavu miongoni mwa wagonjwa wa kisukari.

Vidonda vya kisukari huondosha furaha, amani na hupunguza ubora wa maisha ya wagonjwa wengi wa kisukari. Zaidi ya 15% ya wagonjwa wa kisukari hupata vidonda miguuni au mikononi.

Kwanini wagonjwa wa kisukari hupata vidonda?

Ugonjwa wa kisukari huleta madhara mwilini kwa kuathiri  mishipa ya fahamu, mishipa ya damu na kupunguza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.

1. Kwanza huaribu mishipa ya fahamu na hivyo hutoweza kuhisi.  Kwa kuharibu mishipa ya fahamu husababisha sehemu zinazotegemea mishipa hii kutokufanya kazi kwa ufasaha.

Kwa mfano, upungufu / kosefu wa hisia miguuni husababisha mwenye kisukari kutokufahamu kama mguu umekandamizwa kama kubanwa na kiatu na hivyo kupelekea vidonda.

Vile vile kupungua ufanisi wa kazi za mishipa ya fahamu kwenye mishipa ya damu husababisha wangonjwa wa kisukari kupata matatizo ya presha kushuka na upungufu wa nguvu za kiume.

2.  Kisukari pia huaribu mishipa ya damu na -kama tulivyoona- kusababisha hali inayoitwa artherosclerosis. Hatimaye mishipa ya damu huziba haswa ile ya pembeni ya mwili kama vile miguu.

Kukosekana kwa damu maana yake sehemu husika hukosa chakula, hewa safi na kinga. Hivyo sehemu hiyo hufa na kama utapata maambukizi hutapona kwa urahisi. Mara nyingi hii imekuwa sababu kubwa ya wagonjwa wa kisukari kukatwa miguu.

3.  Njia ya tatu, sukari huathiri kinga ya mwili kwa kuharibu na kupunguza muda wa kuishi wa seli zinazopambana na magonjwa. Hali hii husababisha mgonjwa wa kisukari kuwa katika hatari ya kupata magonjwa hasa ya kuambukiza kwa urahisi na kushindwa kutibika kwa wakati.

Kwasababu ya kuharibiwa kwa mishipa ya fahamu, mgonjwa wa kisukari hukosa hisia miguuni.

Ukijumlisha na athari za kisukari kwenye kupunguza kinga na kupunguza kiwango cha damu kwenye miguu, kama mgonjwa akipata kidonda sehemu hizi kidonda hupona kwa shida na mara nyingi hupata maambukizi.

\"\\"\\"\"Vidonda hivi hutokea haswa katika zile sehemu ambazo hukandamizwa wakati unatembea au umesimama au umelala.

Sehemu hizi ni chini ya vidole gumba, na sehemu ya mbele ya nyayo kama inavyoonekana kwenye picha hii.

Haya yote yanaweza kudhibitika kama tahadhari itachukuliwa katika muda muafaka.

Nani Yuko Kwenye Hatari ya Kupata Vidonda Vya Kisukari Miguuni?

Kama tulivyoona, angalau 15% ya wagonjwa wa kisukari hupata vidonda miguuni. Tafiti zinaonesha kwamba wafuatao wako katika hatari ya kupata vidonda ukilinganisha na wagonjwa wengine wanaoougua kisukari. ugonjwa wa mishipa ya pembeni

  • Ikiwa una ugonjwa wa mishipa ya fahamu: utafahamu kama mishipa yako ya fahamu haifanyi kazi sawasawa kama hutokuwa unahisi ktiaka sehemu yeyote ya mguu au kufa ganzi. 
  • Kama hujaweza kudhibiti sukari yako pia unakuwa katika hatari ya kupata vidonda miguuni. 
  • Wanaouvutaji sigara au kutumia tumbaku
  • Wenye kuugua figo kutokana na kisukari.
  • kuwa na vidonda kabla / au kukatwa mguu kwasababu ya kisukari

Ni muhimu kuhakikisha unadhbibiti sukari kwenye damu, na kuacha matumizi ya tumbaku huku ukifuatilia presha yako ya damu.

Tiba ya Vidonda Vya Kisukari Miguuni

Tiba ya vidonda vya kisukari hutegemea kidonda kilipo, athari iliyotokea na sehemu za mwili zilizoharibika. 

Pia, tiba hutegemea kama kidonda hichi kimepata maambukizi na kama maambukizi yameenea mwilini. 

Matibabu pia hujumuisha kudhibiditi kiwango cha sukari huku ukitibu madhara mengine yaliyotokana na kisukari.

Kwahiyo matibabu yataweza kuwa ushauri na ufuatiliaji, kuosha kidonda, matumizi ya dawa za antibiotiki, pamoja na tiba kwa njia ya upasuaji unaoweza kushirikisha matibabu ya mfupa kama ukiwa umeathirika. 

Kusafisha kidonda ili kuondoa uchafu na tishu zilizokufa, kutibu maambukizi, kuhakikisha damu inafika vizuri miguuni pamoja na kunyanyua kidonda ndiyo njia muhimu kutibu vidonda vya kisukari.

Nyanyua mguu wako ili kuzuia maumivu ya vidonda. Kunyanyua mguu ni muhimu kwa aina zote za vidonda vya miguu ya kisukari. Mkandamizo unaotakana na kutembea huongeza wigo wa maambukizi na kusababisha kidonda kukuwa.

Daktari wako anaweza kupendekeza kuvaa vifaa maalum ili kulinda miguu yako.

Madaktari wanaweza kukwangua / kukata tishuiliyokufa au kuondoa taka zingine zinazoweza kusababisha kidonda kuzidi na kuambukizwa.

Maambukizi ni shida kubwa ya kidonda cha mguu na inahitaji matibabu ya haraka. Kila maambukizi yana tiba yake. Hivyo itategemea na majibu ya uchunguzi ambayo daktari wako ataufanya.

Sampuli za Tishu zinazozunguka kidonda zinaweza kutumwa maabara ili kubaini ni dawa gani ya kuua kidonda itasaidia. 

Ikiwa daktari wako anashuku maambukizi makubwa, anaweza kuagiza X-ray ili kuangalia dalili za maambukizi ya mfupa.

Fanya Mambo Haya Kuepuka Vidonda Vya Miguu

Ili kuepuka shida kubwa za mguu ambazo zinaweza kusababisha kupoteza kidole, kiganja au mguu:

1. Kagua miguu yako kila siku. Angalia mikwaruzo, malengelenge, uwekundu, uvimbe, au kucha
matatizo. Tumia kioo cha kukuza ili kuangalia nyayo zako.

2. Osha miguu katika maji ya uvuguvugu, kamwe isiwe moto. Weka miguu yako safi kwa kuosha kila siku. Tumia maji tu ya uvuguvugu – joto ambalo ungetumia kwa mtoto mchanga. Kausha miguu yako na kuipaka mafuta ispokuwa katikati ya vidole. Ili kuepuka maambukizi kutokana na unyevu. 

3. Osha taratibu miguu yako. Osha kwa kutumia kitambaa cha kufulia au sponji. Kausha kwa uangalifu katikati ya vidole.

4. Kata kucha kwa uangalifu. Usikate kucha fupi sana, kwani hii inaweza
kusababisha kucha kuotea ndani.

5. Kamwe usijitibu sugu mwenyewe. Muone mtumishi wa afya akushauri.

6. Tizama viatu vyako ndani kabla ya kuvaa. Kumbuka, miguu yako
inaweza kutokuhisi kokoto au kitu kingine.

7. Vaa soksi na viatu sahihi. Kiatu kisikubane sana au kupwaya sana.

8. Kamwe usitembee bila viatu, hata nyumbani. Kila mara vaa viatu au malapa. Unaweza kujikwaa na kuumia.

9. Dhibiti sukari yako: Hakikisha sukari yako inakuwa katika kiwango kinachokubalika kiafya:

  • Kama umejipima asubuhi wakati hujala basi iwe kati ya 3.5mmol/L-7.0 mmol/L.
  • Kama umejipima baada ya kula basi iwe kati ya 7.0mmol/L-13.0 mmol/L.

10. Usivute sigara. Uvutaji sigara unazuia mtiririko wa damu miguuni mwako.

11. Mhudumu wa afya akague miguu yako mara kwa mara unapokwenda kliniki. Jitengenezee utaratibu wa kumkumbusha daktari anayekuhudumia ili atizame mguu wako. Njia nzuri ni kumuuliza daktari, unauonaje mguu wangu?

Namana Ya Kuepuka Maambukizi Kwenye Kidonda Cha Kisukari

Maambukizi kwenye kidonda cha mguu yanaweza kuzuiwa kwa kufanya yafuatayo:

  • Osha miguu Weka miguu yako safi kwa kuosha kila siku. Tumia maji tu ya uvuguvugu – joto ambalo ungetumia kwa mtoto mchanga. 
  • Safisha ngozi inayozunguka kidonda
  • Wacha kidonda kikavu na kubadilisha bandage mara kwa mara. Hii itategemea na ushauri wa mhudumu wa Afya, lakini unaweza kubadili angalau mara mbili kwa siku.
  • Usikanyagie mguu weney maambukizi. Ni vizuri kama utaweza kuunyanyua
  • Epuka kujichu mguu kama unahisi maumivu na hujui yanasababishwa na nini

Epuka Madhara Ya Kisukari

Vifaa 3 vitakusaidia kudhibiti na kuepuka madhara ya kisukari. Ukiwanavyo unaweza kufahamu kama uko kwenye hatari ya kupata vidonda na madhara mengine. 

Vipimo Muhimu Kufanya Kujikinga na Vidonda

Vidonda vya kisukari vinaepukika. Hata wale waliokatwa miguu wangelifahamu haya wangeweza kuwa wanatembea hivi tunavyoongea kwani wasingekuwa wamepata kidonda na hivyo kuepuka haya yote yalioysababishwa na vidonda. 

Kumbuka sukari inapozidi na kupungua kwa hisia miguuni ukijumlisha na kushuka kwa kinga mwilini ni huongeza hatari zaidi. Hivyo utahitaji kufahamu kiwango chako cha sukari ili upange mkakati wa kuidhibiti na pia kuweza kufahamu kama unahisi kwenye miguu. 

Hivyo utahitaji kipimo cha sukari -glucometer na kipimo cha hisia-monofilament.

Pima kiwango cha sukari kwenye damu: Ili kuweza kufahamu hali y\"\\"Kipimo\"ako ya kisukari na kuweza kuidhibiti pamoja na kudhibiti madhara yake inabidi uwe na mashine yako kuweza kupima sukari kila wakati unapotaka kufanya hivyo

Kupima hisia miguuni haswa sehemu zile zilizokwenye hatari ya kupata vidonda. Ni muhimukufanya kipimo hiki ili \"\\"\\"\"kuhakiki utimamu wa mishipa yako ya faahmu. Hii itakuwezesha kuepuka vidonda ambavyo vinaweza kukusababisha ukatwe mguu.

Kifaa hichi kina nyuzi  mahususi kwa kupima hisia na hivyo kuweza kuelewa hatari uliyonayo- uwezekano wa kuumia bila kuhisi maumivu.

KIfaa kidogo Faida Kubwa

Fahamu kiwango cha presha yako ya damu na chukua hatua stahiki mapema unapotumia kipimo cha chenye teknolojia ya hali ya juu.

Wakati Gani Nimuone Daktari Kuhusu Vidonda vya Kisukari?

Wagonjwa wanaweza kuonesha dalili za ugonjwa wa mishipa ya fahamu au kuziba kwa mishipa ya damu. Muone mtaalamu wa afya ikiwa unaona mabadiliko yafuatayo:

  • maumivu ya miguu au misuli kukamata katika mapaja wakati wa mazoezi ya mwili
  • Miguu kuwaka moto, kufa ganzi au kuwa na maumivu
  • Kupoteza hisia ya mguso au uwezo wa kuhisi joto au baridi vizuri kwenye miguu
  • Mabadiliko ya muonekano wa  miguu kwa muda – kama vile kuwa myeusi
  • Ngozi ya miguu kuwa kavu kupasuka 
  • Mabadiliko ya rangi na joto la miguu
  • Kucha zilizo nene na manjano
  • Kuwa na maambukizi ya fangasi katikati ya vidole
  • Malengelenge,
  • Kidonda,
  • Kidonda au Sugu iliyoambukizwa,
  • Kucha zinazo ota  kwa ndani.

Kukosekana kwa dalili hizi hakumaanishi kwamba hakuna tatizo lolote kwenye mguu.

Endelea kudhibiti sukari yako huku ukiendelea kuchungua miguu yako. .abidi ufuate kanuni ile ya Kagua mguu kila siku hata kama huhisi mabadiliko au maumivu yeyote, na hakikisha unakwenda hospitali kama ua kidonda kisichopona au lenge lenge lisiloisha.

Kwahiyo Nifanyaje?

  • Dhibiti sukari. Ni lazima upime ili uweze kuahamu kiwango cha sukari na kuchukua hatua stahidi kudhibiti.
  • Kuchunguza mguu wako sasa iwe mara kwa mara kama si kila siku
  • Tathmini tiba yako pia ujue kiwango chako cha sukari kila wakati
  • Usidharau mabadiliko yoyote yanayotokea kwenye mguu. 
  • Anza leo kufuatilia afya yako. Pata vifaa muhimu kwa bei ya punguzo la 50,000/=. Bonyeza Ipate leo hapo chini

SAIDIA WENGINE

Tafadhali Like na Kusambaza Ujumbe Huu Kwa Watu Unaofikiri Watanufaika na Ujumbe Huu. Nitafurahi ukitoa maoni yako kuhusu maboresho hapa chini

Scroll to Top