Umuhimu wa kupima presha ni upi?
Ni kipimo gani cha presha ambacho ni sahihi zaidi? Je, nipime shinikizo la damu kwenye mkono wangu juu au kwenye kiganja cha mkono?
Kupima shinikizo la damu ndiyo njia pekee ya kufahamu kama una shinikizo la juu la damu – presha.
Kufuatilia shinikizo la damu kunaweza kukuchochea kutunza afya yako na kumsaidia daktari wako kuelewa viwango vya shinikizo la damu kwa undani zaidi.
Hivyo kuweza kudhibiti na kuepuka madhara ya shinikizo la juu la damu – presha.
Kuna aina ngapi za vipimo vya presha?
Kipimo cha presha kiganjani
Kipimo cha presha mkononi juu
Kuna aina nyingi za vipimo vya shinikizo la damu vinavyopatikana, na inaweza kuwa vigumu kuamua ni ipi inayofaa zaidi kwa mahitaji yako.
Lakini katika soko la vipimo vya presha kwa matumizi ya nyumbani kuna aina mbili za vipimo vya presha vitumiavyo umeme: kipimo cha kiganjani na cha kwenye msuli mkononi karibu na bega.
Huu ndo utakuwa mada ya leo. Huu ndo utakuwa mada ya leo. Ikiwa kipimo cha mkononi juu – kwenye msuli karibu na bega hutumika nyumbani na kimekuwa kikishauriwa kwa sababu ya ufanisi, maswali yamekuwa mengi kuhusu kipimo cha kiganjani
Unapotafuta kipimo cha shinikizo la damu utakachokitumia nyumbani, kumbuka kwamba usahihi ni mojawapo ya vipengele muhimu zaidi vya kuboresha afya yako.
Tafiti zinaonyesha kuwa vipimo vya shinikizo la damu kwenye kiganja cha mkono hutoa matokeo ambayo ni ya kuaminika kama vile vichunguzi vya juu vya mkono.
Hatahivyo, tafiti ikiwemo iliyofanywa na Zeiker, Rogers na wenzao, zimeonesha kwamba kipimo cha kwenye kiganja cha mkono huwa juu kwa kiwango cha 5mmHg zaidi ya kile kinachopima juu.
Nani hashauriwi kutumia kipimo cha presha cha kiganjani?
Vipimo vya shinikizo la damu vya kiganjani havifai kwa wagonjwa walio na ugonjwa wa kisukari, kwani wanaweza kuwa na mishipa iliyoathirika.
Kwakuwa mishipa ya iliyoko juu mkononi haiathiriwa kwa kiwango kikubwa na umri au magonjwa kama kisukari, wazee, wagonjwa wa kisukari wanatakiwa kupima presha yao kwenye mkono juu ili kupata majibu sahihi.
Wakati gani kipimo cha presha cha kiganjani kinaweza kuleta majibu yasiyo sahihi?
Umri: Tunapozeeka, mishipa yetu ya damu inaweza kuwa myembamba kwa sababu ya kukakamaa, au kuwa migumu kutokana na magonjwa kama vile kisukari.
Kusinyaa kwa mishipa huathiri mishipa katika mkono-kiganjani hasa, kwa kuwa iko mbali zaidi na moyo, na kusababisha kipimo kusoma presha kubwa.
Uvutaji wa sigara: Sigara huathiri mishipa ya damu, kwa hiyo inapendekezwa kwamba wavuta sigara wanapaswa kupima presha yao juu kwenye mkono.
Upimaji: Kifundo chako cha mkono lazima kiwe kwenye kiwango cha moyo unapopima kutoka kwenye kifundo cha mkono wako.
Magonjwa ya moyo na mishipa: Matokeo yasiyo sahihi ya kipimo pia hutokea ikiwa una magonjwa yanayoathiri mdundo wa moyo na mabadiliko kwenye mishipa.
Kwakuwa mishipa ya iliyoko juu mkononi haiathiriwa kwa kiwango kikubwa na umri au magonjwa kama kisukari, wazee, wagonjwa wa kisukari wanatakiwa kupima presha yao kwenye mkono juu ili kupata majibu sahihi.
Vipimo vya kwenye kiganja vinamfaa nani haswa?
Vipimo vya presha vya kiganjani huwafaa sana baadhi ya watu wenye mahitaji maalum.
Kwa mfano, baadhi ya watu walio na mikono mikubwa sana wanaokosa saizi ya kafu ya kipimo cha mkononi juu, kupima shinikizo la damu kwenye kiganja cha mkono kunaweza kuwa sawa.
Namna ya kuboresha usahihi wa kipimo
Inafaa kufuata ushauri wa namna sahihi ya kupima presha.
Ukizingatia haya utapta presha sahihi. Kama ilivyo kwa kipimo cha mkononi juu, kipimo cha presha cha kiganjani huwa sahihi vikitumiwa kama ilivyoelekezwa.
Kwa kipimo cha kiganjani cha kuzingatia, pamoja na mambo mengine, ni kuweka kiganja katika usawa wa moyo kama inavyooneshwa kwenye picha
Pima presha kwa usahihi
Bonyeza HAPA kusoma makala itakayokuelekeza namana sahihi ya kujipima presha yako ili upate majibu sahihi.
Kwanini Wagonjwa wa presha hupata madhara?
Fahamu sababu uepuke. Bonyeza HAPA
Namna 3 tunasaidia kudhibiti presha yako
1. AFYAPlans inakuwezesha Kudhibiti na kuepuka madhara ya magonjwa: Ungana na Daktari wako kwa msaada na mwongozo binafsi Kuhusu dawa, VIPIMO, maarifa na ujuzi kukuwezesha kuwa na uzazi salama, tena ukiwa nyumbani. Bonyeza HAPA kujiunga grupu letu. Utachangia TSh. 4,900/= ikiwa ni Offer!
2. Vitabu vya Elimu vinavyokuwezesha kufanya Maamuzi sahihi kuboresha afya yako. Mfano kudhibiti shinikizo la damu na kisukari huku ukila Vyakula unavyovipenda. Bonyeza HAPA kufahamu zaidi
3. Vifaa vya Matibabu ya Nyumbani vinavyokupa amani na uhakika wa afya yako muda wote. Bonyeza HAPA kuvifahamu.
Uko tayari kuboresha AFYA Yako? Tuwasiliane