Shinikizo la Damu ni Nini?
Shinikizo la damu ni msukumo wa damu kwenye kuta za mishipa ya damu wakati inapopita.
Kila wakati moyo unapodunda, husukuma damu kwenye mishipa kwa kutoa shinikizo. Shinikizo la damu ni muhimu kwa usambazaji wa damu yenye oksijeni na virutubisho kwenye viungo muhimu mwilini.
Shinikizo la damu la kawaida ni Ngapi?
Presha ya kawaida ya damu ni 120/80 mmHg. Namba ya juu (120) inaitwa systolic, ambayo ni presha wakati moyo unasukuma damu.
Namba ya chini (80) inaitwa diastolic, ambayo ni presha wakati moyo unapumzika kati ya mipigo. Ikiwa presha yako ni zaidi ya 130/80 mmHg, ni muhimu kuchukua hatua za kudhibiti.
Jinsi ya Kupima na Kutafsiri Vipimo vya Shinikizo la damu
Ili kujua kama una shinikizo la damu, ni muhimu kupima mara kwa mara. Hapa kuna jinsi ya kutafsiri vipimo:
- Chini ya 120/80 mmHg: Shinikizo la damu la kawaida
- 130/80 mmHg au zaidi: Shinikizo la juu la damu au kama inavyoitwa presha
Namna Sahihi ya Kupima Shinikizo la Damu
Kupima shinikizo la damu kwa usahihi ni muhimu ili kupata matokeo sahihi na kuepuka matokeo potofu ambayo yanaweza kusababisha matibabu yasiyofaa.
Matokeo sahihi yanaweza kusaidia katika kudhibiti shinikizo la damu na kuepusha madhara makubwa kama vile kiharusi na magonjwa ya moyo.
Watu wengi wanapima presha vibaya na kupata matokeo ya uongo. Kwa mfano, kupima presha wakati umekaa vibaya au baada ya kula chakula kunaweza kusababisha matokeo ya juu kuliko kawaida.
Kwa kufuata hatua sahihi wakati wa kupima shinikizo la damu, unaweza kupata matokeo sahihi ambayo yatakusaidia kudhibiti afya yako vizuri.
Zingatia Mambo 7 Kujipima Presha Kwa Usahihi
Ili kupata majibu sahihi zingatia mambo 7 wakati unajipima presha mwenyewe:
- Hakikisha Kipimo Hakijakaza Sana wala Kulegea: Kipimo kinapaswa kufungwa angalau sentimeta 2 kutoka kwenye kiwiko. Hakikisha unaweza kuingiza vidole viwili ndani ya cuff bila shida.
- Usile au Kunywa chochote Dakika 30 Kabla ya Kupima: Hii inasaidia kuepuka matokeo yasiyo sahihi yanayotokana na chakula au vinywaji.
- Kojoa Kabla ya Kusoma: Kama umebanwa na mkojo, hakikisha umekojoa kwanza. Mkojo umebanwa unaweza kuongeza presha.
- Kaa Vizuri Kulingana na Kipimo Unachotumia: Hakikisha umekaa kwenye kiti raha mustarehe na egemea kwa mgongo wako. Subiri kwa angalau dakika 5 ukiwa umefunga kifaa mkononi kabla ya kusoma.
- Weka Miguu Miwili Chini na Usikunje Nne: Miguu iliyonyooka husaidia kupata matokeo sahihi.
- Pumzisha Mkono Juu ya Meza katika Usawa wa Kifua: Kama unatumia mashine ya kufunga juu. Kama unatumia kipimo cha kiganjani, kunja mkono na kiganja kiwe usawa wa moyo. Usinyanyue wala kukunja mkono wakati unapopima.
- Usiongee Wakati Unapima Presha: Kuzungumza kunaweza kuathiri matokeo ya kipimo, hivyo ni muhimu kubaki kimya.
Kwa kufuata hatua hizi, unaweza kupima shinikizo la damu kwa usahihi na kupata matokeo ya kweli ambayo yatakusaidia kudhibiti afya yako vizuri.
Kubadilika badilika kwa presha yako kila unapojipima mara nyingi huwa ni jambo la kawaida.
Ni nadra kupata majibu yanayofanana kama umejipima presha kwa nyakati mbili tofauti.
Presha ya mwanadamu hubadilika badilika katika nyakati tofauti au kwasababu tofauti.
Mabadiliko haya hatahivyo yanaweza kuwa ya kawaida au kwasababu ya tatizo. Nini kitakufahamisha aina ya mabadiliko haya? Endelea kusoma.
Vinavyosababisha presha kubadilika
Ugonjwa wa koti nyeupe (white coat hypertension):
Asilimia 20 ya watu wanaopatikana na shinikizo la juu la damu ni kwasababu ya hofu inayopatokea wakati anapimwa na daktari- au anapokuwa mazingira ya hospitali.
Shinikizo la shinikizo la damu lililojificha (masked hypertension):
Cha kushangaza ni kwamba, watu wengine huwa na presha ya kawaida wakiwa hospitali, lakini inaweza kuwa juu nyumbani.
Majira ya siku:
Shinikizo lako la damu hubadilika katika nyakati tofauti za siku. Kwa ujumla ni chini kabisa wakati wa kulala, huongezeka mida ya shughuli, na huanza kupungua tena mida ya jioni. Kwa maana hiyo, inapendekezwa kujipima shinikizo la damu yako katika muda unaofanana kila siku.
Joto:
Presha yako kawaida huwa juu kwenye baridi na chini kwenye joto. Joto baridi hupunguza mishipa yako ya damu, na kuongeza shinikizo inayohitajika kusukuma damu kupitia hizo. Mabadiliko ya hali ya hewa kama unyevu au shinikizo la anga pia huweza kuathiri shinikizo la damu, haswa kwa watu wa miaka 65 na zaidi. Epuka kuvuta sigara, kunywa vinywaji vyenye kafeini au kufanya mazoezi kwa dakika 30 kabla ya kuchukua BP yako, kwani shughuli hizi zinaweza kuathiri joto la mwili wako.
Msongo wa mawazo (Stress)
Changamoto za kila siku zinaweza kusababisha kuongezeka -kwa muda- kwa shinikizo la damu.
Dawa unayotumia inaweza kuathiri shinikizo la damu
Ikiwa unatumia dawa hakikisha unafahamu kama zina athari kwenye presha yako.
Mazoezi huongeza shinikizo la damu
Ni kawaida kuona kuongezeka kwa muda kwa shinikizo la damu wakati wa mazoezi.
Fuata vidokezo haya ili kuepuka kuongezeka kwa presha kama unafanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito
- Tumia fomu sahihi
- Usibane pumzi yako wakati wa kunyanyua
- Lenga kunyanyua uzito mwepesi mara nyingi
- Chukua tahadhari na dalili hizi: kizunguzungu, kupumua kwa shida na maumivu au kubanwa kifua
Kubanwa na mkojo
Shinikizo lako la damu huwa chini wakati kibofu cha mkojo kiko tupu. Shinikizo la damu yako ya systolic (nambari ya kwanza katika usomaji wa shinikizo la damu, kwa mfano 119 / 79mmHg) inaweza kuongezeka hadi 10mm kwa 15mmHg wakati kibofu chako kimejaa.
Vyakula vinaweza kuathiri shinikizo la damu
Vyakula vilivyo na shinikizo la damu-inaweza kusababisha kupanda kwa muda kwa shinikizo la damu.
Vinywaji vyenye Kafeini
Kafeini inapatikana kwenye kahawa, chai, inaweza kusababisha kupanda kwa muda lakini kwa kasi kwa shinikizo la damu.
Nitajuaje Shinikizo la damu la ukweli?
Kama nilivyotambulisha kwenye makala zilizopita, presha ni wastani wa namba. Lakini, ni wastani wa namba zipi?
Wastani huu hutokana na vipimo unavyofanya. Kama utataka kupimia mara tatu utafanya hivi. Utajumlisha namba za juu za kipimo cha pili na cha tatu kisha utagawanya kwa mbili. Hii itakuwa namba yako ya juu. Na utajumlisha namba za chini za kipimo cha pili na cha tatu kisha utagawanya kwa mbili. Hii itakuwa namba yako ya chini.
Kwa mfano, kama umepima kipimo cha presha ukapata majibu haya: Kipimo cha kwanza, 124/82; Kipimo cha pili 130/88 na Kipimo cha tatu 120/86. Presha yako itakuwa kama ifuatavyo.
Namba ya juu itakuwa 130+120=250/2=125. Namba ya chini itakuwa 88+86=174/2=82. Kwahiyo presha yako ni 125/82.
Nichukue tahadhari ipi kwenye haya mabadiliko?
Utafiti mkubwa wa watu wanaotumia dawa ya shinikizo la damu uligundua kuwa tofauti za zaidi ya 14 mm Hg katika usomaji wa shinikizo la damu huongeza 25% iliongeza hatari ya magonjwa ya moyo.
Je, Nitumie Kipimo gani cha presha?
Fahamu uzuri na mapungufu ya baadhi ya vipimo vya presha. Bonyeza HAPA
Namna 3 tunasaidia kudhibiti presha yako
1. AFYAPlans inakuwezesha Kudhibiti na kuepuka madhara ya magonjwa: Ungana na Daktari wako kwa msaada na mwongozo binafsi Kuhusu dawa, VIPIMO, maarifa na ujuzi kukuwezesha kuwa na uzazi salama, tena ukiwa nyumbani. Bonyeza HAPA kujiunga grupu letu. Utachangia TSh. 4,900/= ikiwa ni Offer!
2. Vitabu vya Elimu vinavyokuwezesha kufanya Maamuzi sahihi kuboresha afya yako. Mfano kudhibiti shinikizo la damu na kisukari huku ukila Vyakula unavyovipenda. Bonyeza HAPA kufahamu zaidi
3. Vifaa vya Matibabu ya Nyumbani vinavyokupa amani na uhakika wa afya yako muda wote. Bonyeza HAPA kuvifahamu.
Uko tayari kuboresha AFYA Yako? Tuwasiliane