Dr. Adinan siku zangu za hatari ni zipi? Nimekutana na mpenzi wangu siku ya 6 baada ya hedhi, je atapata mimba?
Kufahamu siku za kupata mimba ni muhimu sana. Sikuwahi kujua hili. Kutokufahamu siku za kupata mimba kumekuwa kukileta huzuni, karaha na wakati mwengine chuki baina ya watu.
Hivi karibuni, msomaji mmoja alinieleza akiwa na huzuni kubwa:
“Nilidhani nipo kwenye siku salama, kumbe nilikuwa kwenye siku za hatari. Nilipata ujauzito bila kupanga.”
Msomaji mwengine wa kike -mwanafunzi, akiwa na hofu aliniomba nimfahamishe kama alikuwa kwenye siku za hatari, kwani alihofia kupata ujauzito! Dr. Adinan nisaidie, niambie tuu, sijui cha kufanya! Je, naweza kupata mimba? Nimemaliza siku zangu tarehe x na leo nimekutana na mpenzi wangu….niambie tafadhali.
Kisa chake kinafanana na cha wanawake na wanaume wengi – aidha wanashindwa kupata ujauzito kwa sababu hawajui lini hasa ni siku za kupata mimba, au wanapata ujauzito bila kutarajia kwa sababu ya taarifa zisizo sahihi.
Mfano mwengine, siku si nyingi, mwanaume mmoja ambaye amefanikiwa kumpatia mpenzi wake ujauzito baada ya kutumia application yetu, hapo kabla alinilalamikia: “Dr. Adinan, nashindwa kuelewa, mke wangu hapati mimba. Tumekuwa tukijaribu kila wakati haswa kwenye siku za hatari lakini hapati ujauzito“
Wote hawa tuliweza kuwasaidia kwa kuwapatia program yetu, UzaziSalam app na au kuwafundisha namna ya kufahamu mzunguko wa hedhi.
Kuelewa mzunguko wako wa hedhi ni mojawapo ya mambo muhimu zaidi unayoweza kufanya kwa ajili ya afya yako ya uzazi.
Wanaotumia UzaziSalama App wanaendelea kunishukuru kwani imewarahishia na kwasasa hawana hofu tena na waliokuwa na huzuni wameweza kupata watoto. Hatahivyo, kama hutaki kununua app leo (ambayo ni bei ya soda – TSh. 1,000/= tu), bado utapata manufaa kwa kujifunza namna ya kufahamu siku za hatari kwa kutumia kalenda.
Upo Tayari Kuacha Kubahatisha?
Jiunge na zaidi ya wanufaika 500 nchini Tanzania wanaotumia AfyaPlan kupanga familia zao kwa uhakika na kujiamini. Weka maisha yako mikononi mwako.
Jinsi Unavyoweza Kuhesabu Siku za Kupata Mimba
Kwa kutumia Mfano wa Mzunguko wa Siku 28, ninakupatia uelewa wa msingi jinsi wataalamu tunavyokadiria siku za hatari. Hatahivyo ni kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28 usiobadilika:
Siku za hatari (Fertile Window) ni takriban siku sita (6) katika kila mwezi. Linategemea uhai wa mbegu ya kiume (hadi siku 5) na uhai wa yai (saa 24).
- Hatua ya 1: Jua Siku Yako ya Kwanza. Weka alama kwenye kalenda siku unayoanza kupata hedhi. Hiyo ndiyo Siku ya 1 ya mzunguko wako.
- Hatua ya 2: Tafuta Siku ya yai kupevuka (kimombo, Ovulation). Katika mzunguko wa siku 28, ovulation hutokea katikati, yaani siku ya 14. (Hesabu siku 14 kutoka Siku ya 1).
- Hatua ya 3: Tambua Dirisha Kamili. Hesabu siku tano (5) nyuma kutoka siku ya ovulation (Siku ya 14). Hii inamaanisha dirisha lako la hatari linaanza Siku ya 9 na kuishia Siku ya 14. Hizo ndizo siku zako za hatari zaidi.
Mwili wako pia hutoa ishara kama mabadiliko ya ute ukeni (unakuwa mweupe na wa kunyumbulika) au maumivu mepesi ya tumbo.
Kwanini Wengi Hawawezi Kukadiria Siku za Hatari kwa Kutumia Kalenda?
Lakini kabla hatujazama kwenye mahesabu, ni muhimu kuelewa kwanini watu wengi wanakosea siku zao za hatari na kuingia kwenye hali ya wasiwasi na taharuki?
Wengi wetu tumefundishwa kukadiria kwa kutumia kalenda ya kawaida, lakini ukweli ni kwamba watu wengi hawafahamu mambo 3 muhimu:
- DHANA POTOFU YA SIKU 28: Je, unafahamu kuwa mzunguko wa “siku 28” ni wastani tu? Wanawake wengi hawana mzunguko huu. Mzunguko unaweza kuwa wa siku 24, 35, au kubadilika kila mwezi. Kutegemea mahesabu ya “kitabuni” ni kama kuvaa kiatu cha mtu mwingine na kutegemea kikutoshe.
- ADUI ANAYEITWA MAISHA: Mzunguko wa hedhi haufuati kalenda kama mashine. Wiki moja tu yenye msongo wa mawazo (stress), mabadiliko ya lishe, safari, au mazoezi makali inaweza kuchelewesha au kuwahiisha siku yai kupevuka (ovulation) bila wewe kujua. Unapokadiria, unakuwa hujazingatia uhalisia wa maisha yako.
- KUNA GHARAMA ZA KUBAHATISHA: Kama umesoma mpaka hapa maana yake wewe unatafuata msaada wa kitaalamu, hutaki kubahatisha. Kukosea kwa siku moja tu kunaweza kumaanisha kupata ujauzito usiotarajiwa au kukosa kupata mimba ambayo umeisubiri kwa muda mrefu.
Je, upo tayari kupata mfadhaiko, huzuni au taharuki kwa kubahatisha kuhesabu siku za kupata hedhi baada ya ujauzito?
Hofu na wasiwasi unaotokana na kutokuwa na uhakika ndiyo sababu hasa teknolojia imeleta suluhisho bora zaidi.
Usiharibu Amani Yako: Usikosee Makadirio
Kama ulivyoona, mahesabu ya kalenda yanategemea mzunguko wako uwe umetulia kama saa, jambo ambalo ni nadra kwa wengi.
Badala ya kuishi kwa wasiwasi na kubahatisha, tumia teknolojia iliyothibitishwa kukuongoza.
AfyaPlan haichukui nafasi ya ushauri wa daktari, bali inakupa zana ya kukusaidia wewe na daktari wako kufanya maamuzi sahihi.
“Tangu nianze kutumia AfyaPlan, nina amani ya akili. Hakuna tena wasiwasi kila mwezi.” – Mtumiaji wa AfyaPlan
Anza Kujiamini Leo!
