Hata Wewe Unaweza Kudhibiti Presha Ndani ya Mwezi 1
Tunakurudishia Amani kwa Kukuepusha na Madhara ya Presha kwa Kukupatia
Kwanza Fahamu Saabu 4 Kwanini Unashindwa Kudhibiti Presha
Ni wagonjwa 23 tu kati ya wagonjwa 100 wanaopata matibabu ya Presha wamefanikiwa kudhibiti presha zao. Hii inamaanisha watu 77 waliobaki, licha ya kuwa wanatibiwa wako kwenye hatari ya kupata madhara makubwa kama vile figo kufeli, moyo kutanuka, au kiharusi (stroke).
Hizi ndizo Changamoto kuu 4 zinazokuweka kwenye Hatari:
Huujui Ugonjwa wa Presha
Athari kubwa ni Kuyumbishwa. Kila mtu anasema lake na wewe unafuata. Ingawa lengo lako ni kuepuka madhara. Miluzi mingi hupoteza mbwa. Lakini kwakuwa umefika hapa sasa uko makini na utafanikiwa.
Ushahidi: Umeugua muda mrefu lakini mpaka sasa unaulizia kama unaweza kuacha dawa presha ikikaa sawa, au hujui nini cha kufanya nyumbani presha yako ikipanda sana. Au kusema “vyakula vya mgonjwa wa presha ni ghali”.
Unavyotakiwa uwe kuanzia leo: Ufahamu timamu wa uhakika unaokuwezesha kufanya mambo na kuona matokeo chanya:
Hufahamu Kiwango Chako cha Presha – Muda mwingi
Athari kubwa: Kupata madhara taratibu na kuyatambua wakati hali imekuwa mbaya.
Ushahidi: Wagonjwa wa kiharusi, figo kufeli wengi hawakuwa wanajua presha zao. Hawana vipimo.
Unavyotakiwa uwe kuanzia leo: Wewe una kipimo? Unajua namba zako? Ili uweze kudhibiti presha vizuri na kuchukua hatua stahiki mapema inabidi ujue namba zako.
Hufanyi Tathmini – Muda mwingi
Athari kubwa: Unajaribu hiki leo na kuacha kesho bila kuona nafuu ya kueleweka. Unagusa tiba hii, unachanganya na ile, unaona inasaidia kidogo lakini baada ya muda presha inapanda tena. Hujui tena nini ufanye na kipi ni sahihi kwako. Huna Uhakika wa chochote ufanyacho.
Ushahidi: Leo presha imepanda, kesho imeshuka. Hujui nini ulifanya jana presha ikashuka ili uendelee nancho au Uache ulichofanya leo.
Unavyotakiwa kuwa: Rekodi na tathmini kila hatua unayoichukuka kudhibiti presha yako. Lengo ni uweze kujua hatua ipi imeweza kudhibiti presha na uendelee nayo kama ilivyo, au hatua ipi imeonesha ufanisi kidogo hivyo uifanyie marekebisho na hatua ipi uachane nayo kwani haina mchango wowote.
Tatizo Lililojificha
Athari kubwa: Hatari ya madhara na kukata tamaa kwa kuhisi kuwa ugonjwa huu hauna suluhu licha ya kujitahidi kwako kote.
Ushahidi: Kama unafanya haya yote: Una uelewa sahihi, unafanya unachotakiwa kufanya, unafanya tathmini na kubadili mbinu lakini bado presha yako iko pale pale, kuna tatizo lililojificha ambalo bado hujaligundua.
Unavyotakiwa kuwa: Mambo yote haya yamefanyiwa utafiti na kuhakikiwa na wataalamu (hata sisi kwenye tafiti zetu tumehakiki). Hivyo kama hujashusha presha kuna shida hujaibaini. Kinachotakiwa ni wewe na mhudumu wako wa afya kuweza kubaini changamoto ni ipi na namna ya kuikabili.

Dr. Adinan MD, MSc, Fellow Fogarty
Mtafiti wa Magonjwa ya Presha, Kisukari na Moyo | Mbobezi wa Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya
Tangu mwaka 2014, Dr. Adinan amekuwa mstari wa mbele kutafiti na kufundisha wagonjwa kwa mafanikio makubwa katika masuala ya kudhibiti magonjwa sugu ya mfumo wa maisha.
Hivi sasa, anaongoza timu yenye uweledi wa hali ya juu, ari, na kujituma kwa dhati kuhakikisha kila mteja anapata huduma ya karibu na matokeo yanayothibitika.
Mafanikio ya Wateja Wetu Kufikia Sasa
Huduma na Nyenzo 4 Tunazozitumia Kukusaidia Kudhibiti Presha Nyumbani
Huna Uhakika na Presha yako sasa? Hujui vyakula vya kushusha Presha? Umeshindwa Kufuatilia kitaalamu? Hustahili kuishi kwa hofu au kucheza bahati nasibu na afya yako. Tumeunganisha teknolojia na elimu bora ya tiba ili kukupa ulinzi usiotikisika dhidi ya kiharusi na kufeli kwa viungo.
Tunakuwezesha Kufahamu Presha Yako kwa Uhakika
Kipimo hiki cha kisasa kabisa kina viwango vya kimataifa vya usahihi (ISO & CE Certified). Kinakupa majibu ya haraka na sahihi ya sekunde chache ukiwa nyumbani kwakoβbila haja ya kupanga foleni ndefu au kulipia gharama za hospitali kila siku. Ni rahisi kutumia hata kwa wazee!
- β‘ Majibu ya Uhakika & Ya Haraka (Instant Accuracy)
- π MΩumo wa Kidigitali Rahisi Kutumia Mwenyewe
- π‘οΈ Kinakutahadharisha Hali ya Hatari Mapema Sasa
Tunakuwezesha Kudhibiti Presha kwa Vyakula
Acha kuacha kula vyakula unavyovipenda kwa hofu isiyo na msingi! Mwongozo huu wa kitiba unakufundisha siri za kisayansi za mchanganyiko wa vyakula vya asili vinavyoshusha na kuweka presha kwenye kiwango salama kwa kufuata ratiba sahihi na yenye ladha nzuri.
- π₯ Ratiba ya Mlo wa Wiki Nzima ya Vyakula vya Kitanzania
- β Vyakula Vinavyoshusha Presha & Vinavyopaswa Kuepukwa
- π Mfumo wa PDF Utakaosoma Kwenye Simu Yako Wakati Wowote
Tunakuwezesha Kufuatilia Presha Yako Kitaalamu
KIPA App ni kiganja chako cha afya! Inakusaidia kutunza na kufuatilia takwimu za presha yako kila siku, kushiriki kwenye darasa la afya na elimu endelevu, pamoja na kupata fursa ya kujadiliana na kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa Dr. Adinan na wataalamu wenzake.
- π± Rekodi na Fuatilia Trend ya Presha Yako Kila Siku
- π Mfumo wa Madarasa & Masomo ya Afya Endelevu
- π¨ββοΈ Mawasiliano na Majadiliano ya Moja kwa Moja na Daktari
Gundua Chanzo Kilichojificha Kinachokwamisha Udhibiti Wako
Unahitaji huduma hii kama umefanya yote kudhibiti presha mwenyewe lakini unashindwa. Lengo hapa ni kukuepusha na madhara ya presha kwa haraka kwa kugundua na kushughulikia sababu inayofanya usidhibiti presha. Utapata mwongozo wa karibu wa kufuatilia afya yako pamoja na timu ya wataalamu wa afya.
- π©Ί Timu Kamili: Daktari, Muuguzi & Mtaalamu wa Tiba Lishe
- π§ Ushauri wa Kisaikolojia & Wataalamu wa Mazoezi
- π― Kutambua Chanzo Kilichojificha Kinachokwamisha Udhibiti Wako




