Masharti na Faragha – UzaziSmart

1. Masharti ya Matumizi

1. Asili ya Huduma

UzaziSmart ni programu ya kutoa elimu na kutunza kumbukumbu za mzunguko wa hedhi na ujauzito. SIO kifaa cha matibabu na haitoi utambuzi (diagnosis).

2. Kanusho la Kimatibabu

Daima tafuta ushauri wa daktari. Usipuuze ushauri wa kitaalamu kwa sababu ya taarifa ulizosoma kwenye programu hii.

2. Sera ya Faragha

5. Ukusanyaji wa Data

Tunakusanya jina, barua pepe, na taarifa za afya (mzunguko wa hedhi) unazozingiza kwa hiari yako.

6. Matumizi ya Data

Data hizi hutumika kukupa makadirio binafsi ya kalenda yako na kuboresha uzoefu wako ndani ya App.

8. Uhifadhi wa Data (Data Retention)

Muda wa Uhifadhi: Tunahifadhi taarifa zako binafsi kwa muda mrefu kadiri akaunti yako itakapokuwa hai au kwa muda unaohitajika ili kukupa huduma zetu.

  • Baada ya Kufuta Akaunti: Ukiamua kufuta akaunti yako, data zako zote za afya na taarifa binafsi zitafutwa kabisa kwenye seva zetu ndani ya siku 30, isipokuwa kwa taarifa ambazo kisheria tunatakiwa kuzitunza (kama kumbukumbu za malipo).
  • Data zisizotumika: Ikiwa akaunti yako haitotumika kwa zaidi ya miaka 2, UzaziSmart ina haki ya kufuta data zako baada ya kukupa taarifa kupitia barua pepe.

7. Usalama wa Data

Tunatumia teknolojia ya usimbaji (encryption) kulinda data zako dhidi ya ufikiaji usioruhusiwa.

9. Udhibiti wa Mtumiaji

Una haki ya kuhariri, kupakua, au kufuta data zako wakati wowote kupitia mipangilio ya akaunti yako.

10. Mawasiliano

UzaziSmart © 2026

Powered by AFYATech Tanzania

Scroll to Top