PreshaPlan

Hata Wewe Unaweza Kudhibiti Presha Ndani ya Mwezi 1

Tunakurudishia Amani kwa Kukuepusha na Madhara ya Presha kwa Kukupatia

πŸ“š Elimu Sahihi
πŸ₯— Maamuzi sahihi kwa wakati
πŸ“Š Tathmini ya Ufanisi

Kwanza Fahamu Saabu 4 Kwanini Unashindwa Kudhibiti Presha

Ni wagonjwa 23 tu kati ya wagonjwa 100 wanaopata matibabu ya Presha wamefanikiwa kudhibiti presha zao. Hii inamaanisha watu 77 waliobaki, licha ya kuwa wanatibiwa wako kwenye hatari ya kupata madhara makubwa kama vile figo kufeli, moyo kutanuka, au kiharusi (stroke).

Hizi ndizo Changamoto kuu 4 zinazokuweka kwenye Hatari:

1

Huujui Ugonjwa wa Presha

Athari kubwa ni Kuyumbishwa. Kila mtu anasema lake na wewe unafuata. Ingawa lengo lako ni kuepuka madhara. Miluzi mingi hupoteza mbwa. Lakini kwakuwa umefika hapa sasa uko makini na utafanikiwa.

Ushahidi: Umeugua muda mrefu lakini mpaka sasa unaulizia kama unaweza kuacha dawa presha ikikaa sawa, au hujui nini cha kufanya nyumbani presha yako ikipanda sana. Au kusema “vyakula vya mgonjwa wa presha ni ghali”.

Unavyotakiwa uwe kuanzia leo: Ufahamu timamu wa uhakika unaokuwezesha kufanya mambo na kuona matokeo chanya:

2

Hufahamu Kiwango Chako cha Presha – Muda mwingi

Athari kubwa: Kupata madhara taratibu na kuyatambua wakati hali imekuwa mbaya.

Ushahidi: Wagonjwa wa kiharusi, figo kufeli wengi hawakuwa wanajua presha zao. Hawana vipimo.

Unavyotakiwa uwe kuanzia leo: Wewe una kipimo? Unajua namba zako? Ili uweze kudhibiti presha vizuri na kuchukua hatua stahiki mapema inabidi ujue namba zako.

3

Hufanyi Tathmini – Muda mwingi

Athari kubwa: Unajaribu hiki leo na kuacha kesho bila kuona nafuu ya kueleweka. Unagusa tiba hii, unachanganya na ile, unaona inasaidia kidogo lakini baada ya muda presha inapanda tena. Hujui tena nini ufanye na kipi ni sahihi kwako. Huna Uhakika wa chochote ufanyacho.

Ushahidi: Leo presha imepanda, kesho imeshuka. Hujui nini ulifanya jana presha ikashuka ili uendelee nancho au Uache ulichofanya leo.

Unavyotakiwa kuwa: Rekodi na tathmini kila hatua unayoichukuka kudhibiti presha yako. Lengo ni uweze kujua hatua ipi imeweza kudhibiti presha na uendelee nayo kama ilivyo, au hatua ipi imeonesha ufanisi kidogo hivyo uifanyie marekebisho na hatua ipi uachane nayo kwani haina mchango wowote.

4

Tatizo Lililojificha

Athari kubwa: Hatari ya madhara na kukata tamaa kwa kuhisi kuwa ugonjwa huu hauna suluhu licha ya kujitahidi kwako kote.

Ushahidi: Kama unafanya haya yote: Una uelewa sahihi, unafanya unachotakiwa kufanya, unafanya tathmini na kubadili mbinu lakini bado presha yako iko pale pale, kuna tatizo lililojificha ambalo bado hujaligundua.

Unavyotakiwa kuwa: Mambo yote haya yamefanyiwa utafiti na kuhakikiwa na wataalamu (hata sisi kwenye tafiti zetu tumehakiki). Hivyo kama hujashusha presha kuna shida hujaibaini. Kinachotakiwa ni wewe na mhudumu wako wa afya kuweza kubaini changamoto ni ipi na namna ya kuikabili.

Dr. Adinan MD.MSc.Fellow.Fogarty
10+ Miaka ya Uzoefu
Kiongozi na Mtaalamu Mkuu

Dr. Adinan MD, MSc, Fellow Fogarty

Mtafiti wa Magonjwa ya Presha, Kisukari na Moyo | Mbobezi wa Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya

Tangu mwaka 2014, Dr. Adinan amekuwa mstari wa mbele kutafiti na kufundisha wagonjwa kwa mafanikio makubwa katika masuala ya kudhibiti magonjwa sugu ya mfumo wa maisha.

Hivi sasa, anaongoza timu yenye uweledi wa hali ya juu, ari, na kujituma kwa dhati kuhakikisha kila mteja anapata huduma ya karibu na matokeo yanayothibitika.

πŸ”¬ Utafiti Uliothibitishwa
πŸ₯ Utaalamu wa Mifumo ya Afya
πŸ‘₯ Timu Iliyojitolea
Matokeo Yaliyothibitishwa

Mafanikio ya Wateja Wetu Kufikia Sasa

0+ Tuliowasaidia
0+ Waliodhibiti
0% Mafanikio
SULUHU YAKO KAMILI NA YA KITAALAMU

Huduma na Nyenzo 4 Tunazozitumia Kukusaidia Kudhibiti Presha Nyumbani

Huna Uhakika na Presha yako sasa? Hujui vyakula vya kushusha Presha? Umeshindwa Kufuatilia kitaalamu? Hustahili kuishi kwa hofu au kucheza bahati nasibu na afya yako. Tumeunganisha teknolojia na elimu bora ya tiba ili kukupa ulinzi usiotikisika dhidi ya kiharusi na kufeli kwa viungo.

Nyenzo Na. 1

Tunakuwezesha Kufahamu Presha Yako kwa Uhakika

Kipimo hiki cha kisasa kabisa kina viwango vya kimataifa vya usahihi (ISO & CE Certified). Kinakupa majibu ya haraka na sahihi ya sekunde chache ukiwa nyumbani kwakoβ€”bila haja ya kupanga foleni ndefu au kulipia gharama za hospitali kila siku. Ni rahisi kutumia hata kwa wazee!

  • ⚑ Majibu ya Uhakika & Ya Haraka (Instant Accuracy)
  • πŸ”‹ Mفumo wa Kidigitali Rahisi Kutumia Mwenyewe
  • πŸ›‘οΈ Kinakutahadharisha Hali ya Hatari Mapema Sasa
Nyenzo Na. 2

Tunakuwezesha Kudhibiti Presha kwa Vyakula

Acha kuacha kula vyakula unavyovipenda kwa hofu isiyo na msingi! Mwongozo huu wa kitiba unakufundisha siri za kisayansi za mchanganyiko wa vyakula vya asili vinavyoshusha na kuweka presha kwenye kiwango salama kwa kufuata ratiba sahihi na yenye ladha nzuri.

  • πŸ₯— Ratiba ya Mlo wa Wiki Nzima ya Vyakula vya Kitanzania
  • ❌ Vyakula Vinavyoshusha Presha & Vinavyopaswa Kuepukwa
  • πŸ“– Mfumo wa PDF Utakaosoma Kwenye Simu Yako Wakati Wowote
Nyenzo Na. 3

Tunakuwezesha Kufuatilia Presha Yako Kitaalamu

KIPA App ni kiganja chako cha afya! Inakusaidia kutunza na kufuatilia takwimu za presha yako kila siku, kushiriki kwenye darasa la afya na elimu endelevu, pamoja na kupata fursa ya kujadiliana na kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa Dr. Adinan na wataalamu wenzake.

  • πŸ“± Rekodi na Fuatilia Trend ya Presha Yako Kila Siku
  • πŸŽ“ Mfumo wa Madarasa & Masomo ya Afya Endelevu
  • πŸ‘¨β€βš•οΈ Mawasiliano na Majadiliano ya Moja kwa Moja na Daktari
Huduma Na. 4

Gundua Chanzo Kilichojificha Kinachokwamisha Udhibiti Wako

Unahitaji huduma hii kama umefanya yote kudhibiti presha mwenyewe lakini unashindwa. Lengo hapa ni kukuepusha na madhara ya presha kwa haraka kwa kugundua na kushughulikia sababu inayofanya usidhibiti presha. Utapata mwongozo wa karibu wa kufuatilia afya yako pamoja na timu ya wataalamu wa afya.

  • 🩺 Timu Kamili: Daktari, Muuguzi & Mtaalamu wa Tiba Lishe
  • 🧠 Ushauri wa Kisaikolojia & Wataalamu wa Mazoezi
  • 🎯 Kutambua Chanzo Kilichojificha Kinachokwamisha Udhibiti Wako
Chagua Njia Sahihi ya Kudhibiti Presha Yako Anza safari yako leo kwa kuchagua huduma au nyenzo inayokufaa.
Chagua Huduma Hapa βž”
Share
WhatsApp
Scroll to Top