Matibabu ya kisukari ya awali
Metformin ni dawa ambayo daktari wako atakuanzishia kama hutoweza kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kwa njia ya lishe na mazoezi.
Daktari wako ataanza na dozi ndogo na ikibidi atakuongezea dozi mpaka pale atakapohakikisha kwamba sasa kiwango cha sukari kwenye damu kimedhibitiwa.
Uzuri wa metformin ni kutokusababisha ongezeko la uzito au kushusha sukari kwa kiwango kikubwa (hypoglycemia) na ndiyo matibabu ya awali yaliyopendekezwa.
Nani hawezi kutumia metformin?
- Watu walio na ugonjwa sugu wa figo
- Watu wenye ugonjwa wa ini – daktari atathibitisha
- Watu wenye ugonjwa wa moyo – daktari atathibitisha
- Watu wenye matatizo ya kupumua – daktari atathibitisha
- Watu wanaotumia pombe kupindukia
- Kama umeshauriwa na daktari usitumie
Wakati gani mgonjwa wa kisukari huongezewa dawa?
Ikiwa metformin, mazoezi na lishe vitashindwa kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu, daktari wako itabidi akuongezee dawa aina ya sulfonylureas na ikibidi unaweza kuanzishiwa insulin.
Sulfonylurea ya kizazi cha pili (ikiwezekana gliclazide)
Hizi ni dawa kundi lingine ambazo pia hupunguza kiwango cha sukari kwenye damu.
Dawa hizi zinaweza kutumika kama matibabu ya awali wakati huwezi kutumia metformin kwa sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kuhimili maudhi ya dawa (side effects).
Unapotumia Sulfonylureas unaweza kuongezeka uzito au kushuka kwa sukari kwa kiwango cha chini (hypoglycemia).
Lakini ni matumaini yangu kwamba hali hii haitakutokea wewe na hata ikitokea utaweza kuidihibiti kwani wewe ni makini na nitakupatia mbinu nyingi za kuweza kudhibiti madhara ya kisukari.
Nani asitumie Dawa aina ya Glibenclamide kama tiba ya kisukari?
- Watu wenye umri wa miaka 60 au zaidi
- Watu wenye ugonjwa wa ini
- Kwa wagonjwa watakaopata madhara ikiwa sukari yao itashuka sana (hypoglycemia) watu walio katika hatari ya kuanguka, ambao wana ufahamu mdogo wa hypoglycemia, na wanaoishi peke yao
- Madereva au wanaoendesha mashine kama sehemu ya kazi yao.
Dawa zingine za kifamasia hazijaonyeshwa kuwa bora kuliko metformin au sulfonylurea kwa udhibiti wa kiwango cha sukari kwenye damu na matokeo ya muda mrefu ya mgonjwa. Kwahiyo, kwasasa huna haja ya kuanza kufuikiri kutafuta dawa zingine.
Namna ya Kutathimini tiba yako ya kisukari
Si kwa wagonjwa wote tutagemea kushusha sukari yao mpaka kufikia katika kiwango cha kawaida au kuwa karibu ya kawaida.
Hii ni kwasababu unaweza kujikuta umeshusha sukari mpaka kiwango cha chini kabisa na hivyo kuleta madhara. Kumbuka kwamba uko katika matibabu ya kushusha sukari.
Kama ungependa kufahamu namna ya kutathmini tiba yako kama inafanya kazi, au umekuwa ukijiuliza ushushe sukari kwa kiwango gani, au ungeridhika sukari ikifikia kiwango gani? Pata majibu.
Umejiuliza maswali ya muhimu sana kwasababu ndiyo yatakayoamua hatma ya tiba na afya yako kwa ujumla.
Kama nilivyodokeza hapo juu, katika tiba hii tunaweka mizani kuhakikisha sukari haizidi na kuleta madhara, pia hautuishushi sana kwani pia huwa na madhara mabaya kabisa.
Haya yote yatategemea na hali ya mgonjwa, ukali wa ugonjwa, umri wa mgonjwa, uwezekano wake wa sukari yake kushuka pamoja na dawa anazotumia.
Daktari wako atakuelekeza kutoa damu kwa ajili ya kupima kipimo cha HbA1C kuweza kutathmini matibabu yako.
Hatahivyo, anaweza kutumia mashine kama unayotumia nyumbani (Kama huna hakikisha unapata yako boss kwani itakusaidia kufanya tathmini ya tiba yako ukiwa nyumbani) kupima kiwango cha sukari kwenye damu.
Ili kusema tiba yako imekaa sawa sawa na unafikia lengo, majibu ya vipimo vyako yanatakiwa kuwa kama ifuatavyo:
- Wagonjwa wengi wanaweza kutarajiwa kulenga HbA1c ya 7.0%
- Lengo la HbA1c linaweza kupunguzwa (k.m. hadi <8% au kwa watu wenye hatari ya sukari yao kushuka mara kwa mara, au ambao ni wagonjwa sana.
- Wagonjwa wanaotibiwa na lishe, shughuli za mwili na metformin (hatari ndogo sana ya hypoglycemia) wanapaswa kuhimizwa kufikia lengo la chini la HbA1c (Chini ya 7).
- Ikiwa kipimo cha HbA1c hakipatikani Kiwango cha sukari masaa 6 baada ya kula ya chini ya 7.0 mmol/L na kiwango cha sukari masaa 2 baada ya kula ya chini ≤9.0 mmol/L