Dr. Adinan – Msaada wa Kisukari

Je, Unaishi kwa Hofu ya Kisukari?

Pata suluhisho la kisayansi la kudhibiti sukari yako na kurejesha furaha ya maisha.

Wagonjwa wengi wa kisukari hupitia changamoto nzito: kukosa taarifa sahihi, kuhangaika kutafuta dawa bila mafanikio, na hatimaye kukata tamaa. Tafiti zinaonesha kuwa hata wale wanaotumia dawa hupata madhara makubwa kama figo kufeli au ulemavu wa miguu kutokana na vidonda visivyopona.

“Kama nawe unahofu, umefika sehemu salama. Mimi ni Dr. Adinan, na nipo hapa kukusaidia.”

Mambo 3 Tunayopaswa Kukubaliana

Ili nikupe msaada wenye matokeo, ni lazima tukubaliane haya:

  • 1. Ukweli wa Kisayansi: Kwa sasa, kisukari cha aina ya kwanza na ya pili hakina “dawa ya kuponyesha kabisa” (cure), bali kinadhibitika.
  • 2. Udhibiti Unawezekana: Ugonjwa huu unaweza kutawalika ukifuata mfumo sahihi.
  • 3. Unahitaji Mwongozo: Kudhibiti sukari kunahitaji msaada wa kitaalamu na msimamo.

Mkakati Wetu (Tangu 2016)

Mimi ni mtafiti. Kila hatua ninayochukua inapimwa kwa takwimu. Sina sababu ya kukudanganya kwa sababu najua Mungu ananiona, na sitaki uendelee kuteseka. Hapa chini ni mpango wetu wa KIPA:

1. Elimu ya Kweli na Lishe

Tunakufundisha aina ya kisukari ulichonacho ili usipoteze muda kutafuta miujiza. Muhimu zaidi, tunakufundisha kudhibiti sukari kupitia vyakula unavyovipenda.

“Baba yangu alikuwa akisema hawezi kuacha wali, bora afe! Lakini tulimpangia ratiba, akala wali na sukari ikawa salama.”

Pakua Kitabu cha Lishe Hapa

2. Kuchukua Hatua (KIPA Plan)

Tunakusaidia kupanga milo, kupima sukari kwa usahihi, na kufanya vipimo vya moyo na figo ili kuzuia madhara kabla hayajatokea.

Jaza Fomu ya Mpango wa Chakula

3. Ufuatiliaji wa Karibu

Tiba bila ufuatiliaji ni upofu. Kila mtu ana mwili wa tofauti. Kupitia sessions zetu za kila wiki, tunahakikisha hatua tunazochukua zinaleta matokeo chanya.

Fahamu Zaidi Kuhusu Programu Yetu

4. AFYAPlans App (KIPA App)

Teknolojia kiganjani mwako. Rekodi vipimo, pata ushauri wa papo kwa papo, na panga ratiba ya chakula ya wiki nzima kwa kutumia App yetu mahiri.

Pakua KIPA App Sasa

5. Vifaa Tiba vya Nyumbani

Jilinde na madhara ya kisukari kwa kuwa na vifaa bora vya kupimia ukiwa nyumbani.

Pata Vifaa kwa Bei ya Ofa
© 2026 AFYAPlans. Dr. Adinan – Tiba na Takwimu.
Scroll to Top