PreshaPlan

Zaidi ya Asilimia 95% ya Wagonjwa Wetu Wanadhibiti Presha Ndani ya Mwezi 1

Tunakurudishia Amani kwa Kukuepusha na Madhara ya Presha kwa Kukupatia

📚 Elimu Sahihi
🥗 Maamuzi sahihi kwa wakati
📊 Tathmini ya Ufanisi

Kwanini Nimeamua Kusaidia Wagonjwa wa Presha?

Mwaka 2024 nilipokuwa nasoma degree yangu ya Pili, Nilishirikishwa kwenye utafiti wa tathmini kama watu wanaweza kujipima presha kwenye maduka ya dawa Mwanza. Lengo lilikuwa kuboresha ugunduzi wa mapema wa presha ya kupanda ili kuanza matibabu mapema. Alikuja mzee mmoja wa umri wa makamo—ambaye presha yake ilikuwa imepanda kufikia kiwango cha hatari kubwa isiyo ya kawaida ya 215/180 mmHg (Hypertensive Crisis).

💔 “Mwanangu, mbona najisikia vizuri kabisa?”

Nilimmsihi kwa dhati aende hospitali mara moja. Aliniangalia, akatikisa kichwa chake, kisha akatabasamu: “Mwanangu, mbona najisikia vizuri kabisa? Sina dalili yoyote na nina kazi zangu za kufanya.” Aligeuka na kuondoka bila kujua alikuwa anaenda kukutana na mauti.

⚠️ Simu Iliyotikisa Moyo Wangu

Jioni hiyo, simu yangu iliita. Nilipopokea, sauti ya msaidizi wangu wa utafiti ilikuwa ikitetemeka kwa hofu upande wa pili wa simu. Yule mzee alikuwa amepatwa na kiharusi cha kushtukiza (stroke) jana jioni. Alikuwa amelazwa katika wodi ya dharura katika hospitali moja kubwa mjini Mwanza, akiwa hawezi tena kuongezeka wala kujitetea.

🕯️ Muuaji wa Kimya Kimya Asiye na Huruma

Simu hiyo ilinishtua na kuniumiza sana moyoni, lakini pia iliwasha moto mkubwa ndani yangu. Sikuweza kuacha kufikiria jinsi muuaji huyu wa kimya kimya na asiyeonekana anavyonyang’anya familia nguzo zao kwa sababu tu ya ukosefu mdogo sana wa uelewa.

Mzee yule hakukataa matibabu kwa sababu alikuwa mkaidi; alikataa kwa sababu hakuwa anajua. Hakuwa anajua kuwa presha laihitaji kuuma au kutoa dalili ya onyo ili kukupa ulemavu wa kudumu au kuua papo hapo. Hakuwa anajua viwango vyake salama vya presha, hakuwa anajua maana ya kujilinda, wala hakuwa anajua mwamba wa mauti uliokuwa mbele yake.

✊ Kiapo Changu cha Kupambana na Janga Hili

Hapo hapo, niliamua kuwa siwezi kubaki tu pembeni na kuendelea kuhesabu takwimu hizi za majanga ya watu wetu—ilipasa nifanye kitu cha kishujaa kuleta mabadiliko ya kudumu.

Nilipambana na kufanikiwa kupata ufadhili wa utafiti (research grant) mahsusi kwa ajili ya kutatua vikwazo vya ugunduzi wa mapema na udhibiti wa presha ya kupanda. Nilivyoendelea kuchimba kwa undani, ukweli ukawa wazi na wa kuumiza zaidi: ukosefu wa elimu ya afya ni muuaji mkuu nambari moja. Watu hawawezi kudhibiti tatizo ambalo hawalielewi, wala hawawezi kupambana na adui ambaye hawamwoni, haonyeshi dalili, na hasikii maumivu!.

Kuvunja ukimya huo na kuzuia vifo vya kikatili kama vile, tangu 2016 nilianzisha tovuti hii rahisi iliyojitolea kufundisha jamii zetu kuhusu presha na kisukari kwa lugha rahisi wanayoweza kuielewa kikamilifu. Kilichoanza kama kilio na majibu ya dharura ya mchana ule wa huzuni, leo kimekuwa vuguvugu kubwa la kuokoa maisha. Mpaka leo hii tumeshasaidia na kuokoa zaidi ya wagonjwa 1,300.

Dr. Adinan MD.MSc.Fellow.Fogarty
10+ Miaka ya Uzoefu
Kiongozi na Mtaalamu Mkuu

Dr. Adinan MD, MSc, Fellow Fogarty

Mtafiti wa Magonjwa ya Presha, Kisukari na Moyo | Mbobezi wa Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya

Tangu mwaka 2014, Dr. Adinan amekuwa mstari wa mbele kutafiti na kufundisha wagonjwa kwa mafanikio makubwa katika masuala ya kudhibiti magonjwa sugu ya mfumo wa maisha.

Hivi sasa, anaongoza timu yenye uweledi wa hali ya juu, ari, na kujituma kwa dhati kuhakikisha kila mteja anapata huduma ya karibu na matokeo yanayothibitika.

🔬 Utafiti Uliothibitishwa
🏥 Utaalamu wa Mifumo ya Afya
👥 Timu Iliyojitolea
Sifa za Waliofanikiwa

Una Sifa hizi za Mafanikio?:

Baada ya tathmini yetu ya takwimu, nawe unafanikiwa haraka zaidi kwenye PreshaPlan ikiwa una sifa hizi:

Unataka Msaada wa Moja kwa Moja

Umejaribu njia mbalimbali za kudhibiti presha na imeshindikana, ingawa bado unahudhuria kliniki au hospitali mara kwa mara.

Unaamini Ushirikiano na Mtaalamu

Unaamini presha haina tiba ya mkato kwa sasa ila unaweza kuidhibiti, na kwamba ushirikiano wa karibu kati yako na mtaalamu wa afya ndio utakaofanikisha udhibiti huo.

Utayari wa Kuchukua Hatua

Uko tayari kuchukua hatua stahiki kwa wakati kulingana na ushauri wa wataalamu wetu, ikiwemo mabadiliko ya vyakula, mazoezi, na kutathmini afya yako.

Utayari wa Kutumia Zana Tunazoshauri

Uko tayari kujipima na kufuatilia majibu yako. Tutakupatia Kipimo cha Dijitali cha Presha, Kitabu cha Mwongozo wa Vyakula na Kuepuka Madhara, pamoja na KIPA App kwa ajili ya kurekodi vipimo na kupata elimu sahihi.

Matokeo Yaliyothibitishwa

Mafanikio ya Wateja Wetu Kufikia Sasa

0+ Tuliowasaidia
0+ Waliodhibiti
0% Mafanikio
Ratiba ya Mafanikio

Wiki 12 Unapokuwa kwenye PreshaPlan

Hatua kwa hatua kuelekea afya bora na utulivu wa presha yako

WIKI YA 1: Kuanza Safari Yako
Siku ya 1 🩺

Medical Doctor – Tathmini ya Awali

Tathmini ya awali, uchambuzi wa historia ya afya, na mikakati ya awali ya tiba na ufuatiliaji.

Siku ya 2 🍎

Lishe & Vyakula

Uchambuzi wa lishe na mapendekezo ya vyakula sahihi vinavyosaidia kupunguza na kudhibiti presha kulingana na vyakula unavyopendelea na vinavyopatikana ulipo.

Siku ya 3 🧘🏽‍♂️

Mazoezi Salama

Mwongozo wa mazoezi salama yaliyopimwa maalum kusaidia kushusha shinikizo la damu.

Siku ya 4 🧠

Mshauri/Mwanasaikolojia

Mbinu za kisaikolojia na udhibiti wa msongo wa mawazo (stress) unaosababisha presha kupanda.

Siku ya 5 👥

Kukuhakikishia Unaweza!

Kujifunza ushuhuda na mbinu za vitendo kutoka kwa waliofanikiwa kudhibiti presha zao kikamilifu.

Wiki 2 – 12

Vikao vya Ufuatiliaji Kila Wiki

Ufuatiliaji wa karibu na tathmini ya matokeo yako unaofanywa na Daktari pamoja na wataalamu wengine wa afya mara kwa mara inapohitajika hadi kuhakikisha afya yako inatengemaa kikamilifu.

Ushuhuda Halisi

Wanavyosema Waliojiunga!

Tazama jinsi PreshaPlan inavyobadilisha maisha ya watu kote nchini.

⭐⭐⭐⭐⭐

“Nimependa kila kitu kwenye hii PreshaPlan. Wataalamu ni wakarimu sana! Nampenda sana Psychologist wenu.”

JJ
Jane John 📍 Mwanza
⭐⭐⭐⭐⭐

“Nilichopenda kwenye AfyaPlan ni mimi kushauriana na wataalamu wa afya hivyo kushiriki moja kwa moja. Pia timu yenu ina wataalamu wote wanaotakiwa!”

JK
Julia Keys 📍 Moshi
⭐⭐⭐⭐⭐

“Nimefanikiwa kudhibiti presha. Nilikuwa nahofu ya kupata kiharusi. Sasa naweza kufahamu hali yangu kwa uhakika.”

UM
Ussy Mzee 📍 Kilimanjaro
⭐⭐⭐⭐⭐

“Mwanzo nilikuwa na hofu kwamba inafanyika kwenye mtandao (online). Lakini nimejifunza kwamba inanipa uhuru na najidiliana na madaktari kwa wakati muafaka bila kuathiri ratiba zangu.”

MB
Morsa Bilal 📍 Zanzibar
⭐⭐⭐⭐⭐

“Nilichofurahia ni kurudia kula vyakula nilivyokuwa navipenda kwa mpangilio bora bila kuathiri presha yangu sana. Nilikuwa nakula ndizi changa tuu!”

SH
Salim Hashim 📍 Dar es Salaam
⭐⭐⭐⭐⭐

“Vitabu vyenu vizuri na vinaelimisha sana. Pia elimu itolewayo huku ni nzuri na inavutia kwakweli.”

HM
Honest Moshi 📍 Arusha

Epuka Madhara: Changua Mpango wako Sasa.

Chagua mpango unaokufaa leo tuanze safari ya kurejesha amani yako!

Digital Learning & Tracking

Kitabu na KIPA App

Tumia App ya KIPA na Kitabu kuendelea kujifunza, kufuatilia vipimio vyako kiotomatiki na kupima ufanisi wa matibabu yako kwa urahisi.

  • ✅ Kitabu cha Presha na Kisukari
  • ✅ KIPA Mobile App Access (Mafunzo & Mazoezi)
  • ✅ Kufuatilia Vipimio (Presha, Sukari & Uzito)
  • ✅ Kupima Ufanisi wa Matibabu & Ripoti
  • ✅ Elimu ya Lishe na Mfumo wa Maisha
TSh. 75,000/= TSh. 39,000/=
Pata Kitabu na KIPA App (TSh 39,000/=)
Package Kamili

Full PreshaPlan + Vifaa Vyote

Pata kila kitu unachohitaji kuanza safari yako ya kudhibiti presha na kisukari kikamilifu bila kukosa kifaa chochote.

  • ✅ Kipimo cha Presha cha Digitali
  • ✅ Kipimo cha Sukari
  • ✅ Kipimo cha Uzito
  • ✅ Kitabu cha Presha na Kisukari
  • ✅ KIPA Mobile App + Ufuatiliaji wa Daktari
TSh. 280,000/=
Nataka Kujiunga Full PreshaPlan
🔥 Nafasi 5 Tu Zimebaki
Ofa inaisha baada ya Saa: 48:00:00
Chagua Kifurushi Hapo Juu ↑

🔒 Huduma ya Uhakika na Ufuatiliaji wa Karibu

Share
WhatsApp
Scroll to Top