Amani ya Moyo na Uhakika wa Afya Yako ya Uzazi – Kiganjani Mwako

Tunajua umepitia mengi. Umewahi kukaa usiku kucha na maswali mengi moyoni, bila kujua nani wa kumwamini? Hukustahili kupitia hofu hiyo peke yako.

💔 1. Changamoto na Hofu za Wanawake

Kila mwanamke anapitia wakati ambapo anahisi kukwama au kuogopa. Ndio maana tuko hapa kuondoa maumivu haya:

  • Mateso ya Kimya na Aibu: Hofu ya kuuliza maswali kuhusu miwasho, harufu isiyo ya kawaida, au ute usio wa kawaida hospitalini kwa kuogopa kuhukumiwa au kuaibika.

  • Makosa ya Kalenda na Hofu ya Mimba: Mkanganyiko wa kutoelewa mzunguko wa hedhi na siku za hatari, unaopelekea hofu ya mimba za kushtukiza au kutoshika mimba kwa muda mrefu.

  • Kutokusikilizwa na Madaktari: Uchovu wa kwenda hospitalini na kuhudumiwa kwa haraka kama “namba tu”, bila daktari kutumia muda kukusikiliza na kukupa matumaini.

  • Uwezekano wa Kupata Taarifa za Uongo: Kutafuta majibu kwenye mtandao (Google) na kupata majibu yanayozidisha hofu, badala ya ushauri sahihi wa kitaalamu.

  • Hofu ya Safari ya Ujauzito: Wasiwasi wa maendeleo ya mtoto, mabadiliko ya mwili, mood swings, na hofu ya siku ya kujifungua bila kuwa na daktari anayekupigania.
Mwanamke akifurahia baada ya kudhibiti afya yake ya uzazi anapotumia UzaziSmart

🌸 2. Je, Unataka Amani na Kujiamini  

Huduma hii imeundwa mahsusi kwa ajili yako ikiwa wewe ni:

  • Mwanamke Makini ambaye hutumii dawa hovyo bila kujua unatibu tatizo gani.

  • Mwanamke Unayejiamini na hivyo kutaka ushauri kutoka kwa watu unaoweza kuwaamini kulingana na ujuzi na uelewa wao wa mambo.

  • Mwanamke anayejipenda unayetaka kusikilizwa na daktari kwa kituo na kwa undani ili shida yako itatuliwe kikamilifu na kuepuka madhara.

🌸 3. Faida ya kujiunga na UzaziSalama 

Faida tatu muhimu unazopata unapojiunga na UzaziSalama ni:

  • Amani: Unayetaka majibu ya uhakika kuhusu afya yako ya uke na uzazi bila mtu mwingine yeyote kujua.

  • Kujiamini: Unasikilizwa kwa undani, bila kukatishwa mpaka umalize kinachokusibu. Kisha unapata ushauri wa uhakika kutoka kwa daktari mbobezi. Hakuna tena kuhangaika kwenye mitandao kutafuta majibu usiyo na uhakika nayo!

  • Tumia muda wako kufanya shughuli muhimu: Taarifa zote muhimu unazipata kwenye UzaziSmart App. Na ukihitaji, Unapiga simu yako na kujibiwa kitaalamu na daktari mbobezi.
Mwanamke akifurahia baada ya kudhibiti afya yake ya uzazi anapotumia UzaziSmart

💖 3. Vifurushi Vyetu vya Huduma

UzaziSmart App

Msaidizi wa Kidijitali saa 24/7

TSh 5,000 kwa mwaka mmoja
  • Afya ya Wanawake: Uliza maswali wakati wowote.
  • Mzunguko: Fahamu siku zako za hatari.
  • Ujauzito: Kikokotoo cha tarehe ya kujifungua.
  • Uchungu: Tambua dalili za kuanza kwa uchungu.
Jiunge na App
HUDUMA BORA YA UJAUZITO

Darasa & Ushauri

Mwaka Mzima / miezi 9 ya Ujauzito

TSh 29,000 kipindi chote cha ujauzito
  • Ukaribu wa Kiurafiki: Daktari wa kukusikiliza.
  • Darasa la Moja kwa Moja: Kila wiki.
  • Usimamizi kamili mwanzo hadi mwisho.
  • Huduma zote za App zimejumuishwa bure.
Chagua Platinum

Ushauri Binafsi

Maongezi ya siri na Dr. Bingwa

TSh 9,000 kwa mara moja
  • Sikilizwa kwa makini kuhusu tatizo lako.
  • Ushauri wa haraka na wa kitaalamu.
  • Suluhisho la changamoto za afya ya uzazi.
  • Maelekezo rasmi ya kitabibu (Prescription).
Pata Ushauri

❓ Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs)

Bonyeza swali lolote kupata majibu ya kina kutoka UzaziSalama.

Hapana, sisi si hospitali ya kawaida ya majengo.

UzaziSalama ni huduma ya kidijitali iliyoanzishwa baada ya kuona changamoto wanazopitia wanawake kama wewe—wanawake wanaojali afya zao lakini wanahitaji huduma ya faragha, ya haraka, na ya ukaribu bila kupanga foleni. Tunatumia simu na mtandao kukusogezea daktari bingwa popote ulipo.
Usijali kabisa, huduma yetu haina mipaka ya kijiografia!

Popote ulipo nchini—iwe upo jijini au kijijini—huduma yetu inakufikia kupitia simu yako ya mkononi. Hukhitaji kusafiri wala kutoka nyumbani kwako ili kupata ushauri wa daktari bingwa.
Wewe humjui daktari, lakini sisi tunawajua vizuri sana.

Tunakuchagulia daktari mzuri zaidi, mwenye uzoefu wa hali ya juu na moyo wa upendo, ambaye atafurahia kukusikiliza na kukusaidia. Tunahakikisha unakutanishwa na mtaalamu anayeelewa vizuri zaidi aina ya changamoto yako. Uko mikono salama 100%.
Ndio, faragha yako ndiyo kipaumbele chetu namba moja.

Hakuna mtu mwingine yeyote atakayejua au kusikiliza maongezi yako. Kila kitu unachozungumza na daktari kinabaki kuwa siri kubwa kati yako na mtaalamu wako. Ongea kwa uhuru bila hofu ya kuhukumiwa.
Daktari akikushauri kufanya vipimo au kukupa maelekezo ya dawa (Prescription), utakutumia barua au ujumbe rasmi wa kitabibu. Unaweza kwenda na cheti hicho kwenye maabara au duka la dawa (Pharmacy) lililo karibu nawe kupata huduma mara moja.
Huduma yetu ni kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu, ufuatiliaji wa afya, mzunguko, na ujauzito. Kama unapitia dharura kubwa ya kiafya (mfano: kuvuja damu kwa wingi au maumivu makali sana yasiyovumilika), tunakushauri uwahi haraka kituo cha afya au hospitali iliyo karibu nawe kwa msaada wa dharura wa ana kwa ana.
Malipo haya yanakupa fursa ya kufanya maongezi ya kina ya faragha na Daktari Bingwa, kupewa muda wa kutosha wa kusikilizwa, kupata majibu ya kisayansi ya changamoto yako, pamoja na UzaziSmart App kwa muda wa miezi mitatu (3).
Ushuhuda wa Akina Mama

Wanachosema Watumiaji Wetu

Tazama jinsi UzaziSmart inavyobadilisha maisha ya kina mama na familia zao kote nchini.

★★★★★

"Nilikuwa na hofu kubwa na maswali mengi kuhusu afya yangu, lakini maongezi yangu na daktari kupitia mfumo huu yalinipa amani ya moyo. Daktari alinijibu kwa upendo, subira, na kitaalamu sana bila kunifanya nijihisi vibaya."

★★★★★

"Baada ya kuhangaika kwa zaidi ya miaka miwili kutafuta mtoto, UzaziSmart App ilinisaidia kufuatilia siku zangu za hatari kwa usahihi wa hali ya juu. Baada ya miezi mitatu tu ya kutumia miongozo yake, hivi sasa nina ujauzito wa miezi 5!"

★★★★★

"Nilikuwa nahitaji mapumziko kabla ya kupata mtoto mwingine bila kutumia njia zenye madhara kwangu. App hii imenifundisha mzunguko wangu kwa usahihi na kunipa mbinu za kuzuia mimba kwa usalama pindi nilipohitaji kufanya hivyo."

★★★★★

"Elimu ya maendeleo ya mtoto tumboni na tarehe sahihi ya kujifungua ilinisaidia sana kujiandaa vyema. App ilinipa taarifa za kila wiki kuhusu hatua za ukuaji wa mwanangu hadi siku niliyojifungua salama."

★★★★★

"App hii iliokoa maisha yangu na ya mwanangu! Nilipopata dalili fulani, nilikumbuka elimu ya 'Dalili za Hatari' tuliyopewa na kuwahi hospitali haraka. Madaktari walisema kuwahi kwangu ndiko kuliokoa maisha ya mtoto wangu."

Scroll to Top